Sunday, August 21, 2011

SAKATA LA WORKSHOP YA ENTERPRENUERSHIP :MWENYEKITI MUEDA ASHIKILIA MSIMAMO WAKE, WASHIRIKI WADAI PESA ZAO, MUSO YAHUSISHWA NI VURUGU MECHI TUPU!

Kutokana na mvutano ulioibuka siku ya jana kati ya washiriki na viongozi wa MUEDA kutokana na washiriki wa workshop hiyo kulalamika vikali wakidai kutapeliwa tayari hali ya mambo imezidi kuchafuka kabisa.

Akizungumza na blog hii ya MUSO Link mwenyekiti wa MUEDA Bw Baraka Mwilapwa amekanusha vikali kuhusika na ubadhirifu wa aina yoyote, fuatilia mahojiano hayo na mwenyekiti wa MUEDA ili ufahamu undani wa sakata hilo;

MUSO link; Ndugu mwenyekiti wa MUEDA kwanini mmedanganya watu kuwa kuna wanataalamu kama prof kamuzora wangeshiriki lakini hawakuwepo?

Baraka; Hakuna ukweli wowote juu ya hilo isipokuwa ni kweli walisema wangehudhuria lakini kwa bahati mbaya ni kuwa hawakuweza kufika na walinipa taarifa.

MUSO link; Je baada ya wanataaluma hao kusema hawatahudhuria je kwanini hukutoa taarifa kwa washiriki?

Baraka; Nikiri wazi kuwa ni kweli walinipa taarifa lakini nilishindwa kuwajulisha washiriki kwasababu nilihofia kuharibu mood yao.

MUSO link; Kuna baadhi ya washiriki wanadai MUSO inahusika katika sakata hili, je wewe unaliongeleaje?

Baraka; Niseme jambo moja kuwa MUSO haihusikiki na MUEDA hivyo hakuna sababu yoyote ya kuihusisha MUSO na mambo ya MUEDA.

MUSO link; Ndugu Baraka unakubali kuwa kama mwanafunzi ukifanya mtihani unajua aidha umefeli au umafaulu, sasa washiriki wanaona huduma iliyotolewa na pesa walizolipa ni kama kaskazini na kusini, je wewe unasemaje?

Baraka; Jambo pekee naloweza kusema ni kuwa watu walinipongeza sana lakini huo uvumi unaonezwa ni upuuzi wa watu wachache tu ambao walitaka wapewe mambo fulani fulani lakini wamekosa , ni lazima wajue kuwa hii ni taasisi siyo mali ya mtu hivy mambo yanaenda kwa kanuni siyo ushabiki.

MUSO link; Mwishowe unawaambia nini wanamzumbe? na washiriki wote wa workshop?

Baraka; Nawaambia wanamzumbe kuwa kinachomatter ni knowledge siyo misosi hivyo wafurahie kupata mind liberation siyo vitu consumable kama vyakula na vinywaji.

Haya sasa mdau unasemaje kuhusu sakata hili tupe maoni yako...!



No comments:

Post a Comment