Pengine kuna bundi ameanza kulia ofisi ya MUSO, ndiyo ni bundi ndiyo maana tunashindwa kuelewa kuna tatizo gani kati ya Jacob Julius na Uswege Isaac ambao wamewahi kufanya kazi pamoja tena nathubutu kusema "ni marafiki wa siku nyingi hawajakutana njiani tu"
Tunashangazwa na vuta nikuvute ya sasa tena kupitia mtandao wa facebook ambapo Bw Jacob Julius anaendeleza mapambano yake aliyoyapachika jina la "WAR AGAINST UFISADI" huku licha ya kuandika kwa mafumbo wenye uzoefu wa maswala ya uandishi tunaelewa kuwa kwa mlango wa nyuma anailenga MUSO lakini kwa mlango wa mbele anamlenga Uswege, kuamini nayosema hebu soma ujumbe huu.............."Meya Mzumbe
Nashauri utaratibu wa kulipana posho zisizo na tija kwa viongozi wa Chuo uondolewe rasmi,huku ndiko tunakojifunzia uwizi na ufisadi.Imagine mtu yupo likizo kwa sasa lakini kila mwisho wa mwezi anapewa posho ya mawasiliano mana ndivyo Bunge ...lilivyobariki,sasa nauliza mtu huyu anawasiliana na nani wakati yupo likizo?HILI NDILO LILILOSABABISHA MAWAZIRI KUMTISHIA USWEGE KWAMBA WATAJIUZULU ENDAPO HATA NIWAJIBISHA,NAMI NIKAMSHAURI ASIWE NA SHAKA YOYOTE MIMI NIKO FLEXIBLE NA HURU HIVYO AAMUE KULINDA MASLAHI YA SERIKALI YAKE,NAYE AKAONA MASLAHI YA SERIKALI YAKE NI KUNIONDOA BARAZANI,NI JAMBO JEMA TENA LA KHERI ILA SASA TUTAHITAJI MJADALA WA WAZI KUJADILI HAYA MAPOSHO WANAYOLIPANA KILA MWISHO WA MWEZI MANA BADO HAIJANIINGIA AKILINI KABISA"
No comments:
Post a Comment