Monday, September 12, 2011

Jamii Forums(JF) Waendelea Kumchafua Dr Mbwambo wa Mzumbe University!

Dr Mbwambo
Mtandao maarufu wa Habari wa Kijamii wa Jamii Forums maarufu kama JF unadaiwa kuendeleza msimamo wake wa kumchafua Dr Andrew Mbwambo ambaye ni Dean wa School of Business tawi la Mzumbe la jijini Dar es salaam kuwa hana PHD.

Taarifa za uhakika ambazo Blog hii inazo zinaonyesha kuwa ujumbe huo unaodaiwa kumchafua Dr Andrew Mbwambo uliopachikwa jina la "Je "Dr" Mbwambo wa Mzumbe University Dar Business School ame-graduate PhD yake?",  ujumbe huo ambao umechapwa tangu tarehe 6th April 2009  muda 19:16 p.m kwa saa za Afrika Mashariki unaendelea kudai hivi "Kwa Wadau Wote: Kwa kuwa naamini kuwa inawezekana naweza kuwa nakosea, na kuwa nimesikia au najua kupitia vyanzo mbalimbali kuwa anayejiita "DR" MBWAMBO, ambaye ni Dean wa Mzumbe University Dar Business School, hajamaliza bado PhD yake huko Nairobi University...naombeni uelewa wenu katika hili. Na kama bado, ina maana gani? na Ina picha gani kwa Mzumbe University kwa ujumla? Hili si jungu...ni utafutaji wa ukweli...

Mkereketwa! "


Haijaeleweka  mara moja lengo la mwandishi wa habari hiyo ambaye hata hivyo anatumia jina bandia la "qwerty3 ", madai haya yanaendelea kukumbatiwa na mtandao huo kwa zaidi ya miaka miwili sasa huku tukiwa na taarifa rasmi kuwa anayeitwa Dr Mbwambo ni kweli ni PHD Holder ambaye ulimwengu mzima unamtambua kuwa ni msomi mwenye kiwango hicho cha juu cha elimu yaani PHD.

Tunadhani huu ni mwanzo mzuri kwa Dr Mbwambo na Chuo Kikuu Mzumbe kulifatilia sakata hili ambalo kwa namna moja au nyingine linamchafua msomi huyo na Chuo kikuu Mzumbe.

BLOG HII INATOA POLE KWA DR MBWAMBO KWA ATHARI ZOTE ZINAZOSABABISHWA NA UZUSHI HUU NA PROPAGANDA HIZI CHAFU.

No comments:

Post a Comment