Thursday, August 25, 2011

Hotuba ya Waziri wa Fedha; Matumaini Kibao!

Waziri wa fedha wa MUSO Mh Alex Getang'ita akisoma hotuba yake Bungeni

MZUMBE UNIVERSITY STUDENTS ORGANIZATION (MUSO)

MINISTRY OF FINANCE, PLANNING AND INVESTMENT.



HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHESHIMIWA GETANG’ITA ALEXANDER NYANCHINI (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2011/2012.

TAREHE 22-08-2011

UTANGULIZI:                               

1. Mheshimiwa spika,naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu likubali kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya serikali ya mwaka wa fedha 2011/2012.Pamoja na hotuba hii yapo majedwali yanayoonyesha makisio ya mapato na matumizi.

2. Mheshimiwa spika, awali ya yote napenda kumpongeza Rais wa serikali ya wanachuo kikuu Mzumbe Mh.Uswege Isaac Mwakabonga, kwa kuchaguliwa kuongoza MUSO akiwa rais wa awamu ya kumi. Aidha ninamshukuru sana mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyonayo kwangu kwa kunichagua kuongoza wizara kubwa na nyeti, ninamuahidi kuwa sitamuangusha. Pia ninampongeza Mh.Happy Joseph kwa kuchaguliwa kuwa makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe. Vilevile naendelea kutoa pongezi kwa  Mh. Benson Fute (Mb),kwa kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe. Natoa ahadi ya kushirikiana naye kwa karibu kama mtendaji mkuu wa serikali katika kuhakikiksha tunatenda yale yote Rais aliyotuamini kwayo.

3.Mheshimiwa spika, napenda kukupongeza wewe binafsi kwa kuchaguliwa kuwa spika, na hivyo kuwa mwanachuo wa kwanza wa shahada ya pili (masters) kuongoza bunge hili tangu chuo hiki kilipopata hadhi ya kuwa chuo kikuu.Kuchaguliwa kwako kunatokana na imani kubwa waliyonayo waheshimiwa wabunge kwa kuzingatia busara zako,uwezo na uzoefu wako.Napenda pia kumpongeza Mh. Suzan Kuzilwa kwa kuchaguliwa kuwa naibu spika,nawapongeza pia mawaziri wenzangu wote pamoja na Naibu mawaziri wote, kwa kuteuliwa kwao na Mh.Rais kushika nyadhifa hizo. Aidha, napenda niwapongeze wabunge wote kwa kuchaguliwa na kuteuliwa kuwawakilisha wanachuo wenzetu katika bunge hili, chombo ambacho maamuzi makuu yanayohusu ustawi wa wanachuo kikuu Mzumbe.

4. Mheshimiwa Spika,naomba kwa namna ya pekee niwashukuru Mh.Mabula R. Mabula,Naibu waziri wizara ya fedha na katibu mkuu wa wizara ya fedha Mh. Nanzia Rajab kwa kazi ngumu waliyofanya katika kuandaa bajeti hii.

5. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa kazi wanazofanya wawakilishi wa madarasa (CR’S), serikali hii imeonelea ni vyema kuwatia motisha angalau kwa posho kidogo hata za mawasiliano kama kifuta jasho cha kazi nzito wanazozifanya. Hii itakuwa ni serikali ya kwanza tangu chuo hiki kianzishwe, kutoa posho kwa wawakilishi wa madarasa (CR’S). Kulingana na ufinyu wa bajeti yetu, kiasi cha fedha walichotengewa si kikubwa sana lakini ni mwanzo mzuri ambao ninaamini kama serikali zijazo zikiufuata na kuuboresha utaleta tija katika ufanisi wa kazi za hawa waheshimiwa.

6.Mheshimiwa Spika, kwa kipindi kirefu chuo kikuu Mzumbe, kimekuwa kikijiweka kando na masuala ya kitaifa ambayo tumekuwa tukiona vyuo vingine vikijihusisha siku hadi siku, serikali hii imejikita sana katika kuwawezesha wana wanachuo kikuu Mzumbe kushiriki katika masuala ya kitaifa na serikali imejipanga kuhakikisha inafanikisha adhima hii ikishirikiana na menejimenti ya chuo ya chuo kikuu Mzumbe.

7. Mheshimiwa Spika, katika bajeti hii serikali imeweka kipaumbele kuiboresha tovuti, ya MUSO ambayo hadi sasa  iko katika hali nzuri, napenda kumpongeza mheshimiwa Waziri husika kwa kazi nzuri anayoifanya.

8. Mheshimiwa Spika,ninayo furaha pia kusimama hapa mbele ili kutoa matazamio ya serikali kwa upande wa mapato na matumizi kwa kipindi cha mwaka mmoja wa madaraka. Bajeti ninayokwenda kuisoma punde imeangalia nyanja zote muhimu kwa maslahi ya wanafunzi wote wa chuo kikuu Mzumbe na hivyo napenda kutanguliza ombi langu kwa waheshimiwa wabunge kuwa makini sana kuchangia kwa mawazo ya kujenga na hatimaye kuipitisha ili wanafunzi wenzetu ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kutoona matunda ya pesa zao, kupitia bajeti hii, sasa wakapate kuona matunda hayo.

Naomba nichukue fursa hii sasa niweze kusoma makadirio ya mapato na matumizi ya serikali ya chuo kikuu Mzumbe kwa mwaka wa fedha 2011/2012 kwa kuzingatia mchanganuo wa kila wizara.







MHESHIMIWA SPIKA NAOMBA KUTOA HOJA.

No comments:

Post a Comment