Monday, August 29, 2011

Onesmo Mpinzile Atetea Uamuzi Wa Mh Uswege Kumtimua Jacob.......Soma uchambuzi wake wa kisheria

Maamuzi ya Mh Uswege Kisheria

Katika taratibu za kisheria kwa maana ya Both administrative and Constitutional law, Alichokifanya Mh Uswege kinakubalika nisijue kibinadamu! Principle za Ministerial kwa maana ya (Collective na Individual) responsibility Waziri au member yeyote wa cabinet haruhusiwi kupinga jambo au hoja yoyote ya serikali bungeni, anatakiwa kufanya hivyo wakati akiwa kwenye vikao vya Cabinet (Baraza la mawaziri), anatakiwa kuonyesha hali hiyo kwa presiding cabinet chairman amabyo kwa kawaida anaweza kuwa President, Vice president au Prime Minister as the circumstance may be.
Ikiwa jambo hilo au hoja hiyo waziri au member yeyote wa cabinet anaona imeshindikana kukubalika na anaona ina maslahi kwa umma au taifa na imekataliwa kujadiliwa na baraza hilo au imetupiliwa mbali!!...Basi mjumbe huyo wa baraza ataamua kujiudhru uwaziri au ujumbe wa baraza ili ajadili jambo hilo kama mbunge...na katika hali hiyo atakuwa huru kulipinga kwa nguvu zake zote. Kama hatajiudhuru wadhifa huo kwanza na akapinga, sheria inasema kwamba President atatakiwa kumfukuza kazi...Jambo la kumfukuza kazi ni discreationlly (au lipo ndani ya maamuzi ya rais, anaweza kufanya hivyo au asifanye hivyo). Hana obligation (ulazima ) wa kumfuta kazi, n hakuna ulazima wa yeye kufanya hivyo...

Jambo hili si jipya liliwahi kutokea hapa Tanzania na nchi nyngi za jumuiya ya madola, mfano miaka ya 1987-89 Kingunge Ngombale Mwilu wakati akiwa Regional Commissioner, 1993 Mh Augustine Lyatonga Mrema alilazimika kujiudhuru uwaziri kutokana na kutoridhika na maamuzi ya jambo kwenye baraza a mawaziri, Pia angalizo hilo lipo katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, 1977, ambayo inasema 'the Minister shall assume office at the pleasure of the President'.
Hivyo kisheria jambo hilo lipo sahihi nisijue mchango wa Jaju katika baraza la Mh Uswege .

Mpinzile  S. Onesmo
+255714702824
+255785702824
craddleb@yahoo.com
craddletz@gmail.com
Mzumbe University, Bachelor of Laws
Mororogoro Tanzania.

No comments:

Post a Comment