Katika kuonyesha kuwa za mwizi ni arobaini, jamaa mmoja ambaye anakawaida ya kuibuka kwenye sherehe pasipo kualikwa ameumbuka vibaya jana baada ya kuingia kwenye "domo la mamba"
Blo hii ilimfatilia jamaa huyo hatua kwa hatua tangu akipanda Hiace mpaka Morogoro mjini ambapo aliingia kwenye nyumba fulani maeneo ya Kihonda kisha akatoka akiwa amevaa kanzu na ghafla akaingia kwenye uchochoro fulani na kukodi baiskeli kisha safari ya "kuzamia "ikaanza.
Alipofika kwenye sherehe hiyo ambayo hakualikwa jamaaa kapaki baiskeli yake na kukaa mkekani ghafla mgawa chakula na vinywaji alipomfikia akataka kuponi, ghafla jamaa akasema kaisahau basi akahojiwa "twambie hata rangi ya kuponi" jamaa akashindwa akapaniki akataka kupigana, muda wote huo mwandishi wetu alikuwa anamfatilia ndipo jamaa kwa hasira akapanda baiskeli yake na kutokomea.
No comments:
Post a Comment