Friday, August 26, 2011

BREAKING NEEWZ! MH HASSAN MASSAWE HOI MAFOMU YAMDODEA MKONONI BAADHI YA MA-CR WADAI POSHO!

Kama ulidhani uongozi wa MUSO ni lele mama a.k.a cha mtoto basi muulize waziri wa afya Mh Hassan Massawe ambaye amekumbwa na kigingi cha kwanza kutoka kwa ma-cr. Habari za uhakika zinadai kuwa waliomtia mkosi Bw Massawe ni maclass representative kutoka faculty of science and technology ambao ni ICTM, POM na A.S

Habari zinadai kuwa Bw Massawe alikuja na idea yake ya kukusanya maoni kuhusu dispensary na huduma za afya ambapo aliandaa fomu na kuwakabidhi ma cr ili watu wajaze ndipo kinyume na mategemeo yake ma cr wa science na technology wametaka posho kwa madai kuwa wapo busy na kusambaza fomu ni kazi nzito, naye Massawe akajibu kwa hasira kuwa MUSO haina pesa na ma cr wamemsusia, mpaka tunaenda mtamboni usiku huu mafomu ya Bw Massawe yamerundikana pale MUSO Office.

No comments:

Post a Comment