Kama ulikuwa hujui sikia hii kutoka jengo hilo hapo juu kuna sakata la aina yake limetokea Library baada ya jamaa mmoja kunaswa na kamera za Library akikwapua simu.
Taarifa za ndani kutoka kwa chanzo chetu mmoja wa wafanyakazi wa Library zinadai kuwa jamaa huyo ni mwaka wa kwanza ambaye amenaswa live na kamera akikwapua simu hiyo.
Akielezea sakata hilo mfanyakazi huyo wa Library amekaririwa akisema..."mimi nakwambia hivi huyu mtoto ana tatizo gani amekuja huku kusoma au kuiba? "
Habari za utafiti zinaweka bayana kuwa hata serikali ya MUSO inafahamu kuhusu jambo hilo lakini bado haijafahamika ni hatua zipi MUSO imechukua?
Mpaka tunakwenda mtamboni muda huu tuna taarifa rasmi kuwa mhusika wa uhalifu huo tayari ametiwa nguvuni, na mwandishi wetu anafatilia kwa karibu ili kubaini hatua zipi zitachukuliwa dhidi yake.
No comments:
Post a Comment