Tuesday, September 20, 2011

YUNA Mzumbe Hali Si Shwari; Jacob Atupa Lawama Kwa Mwenyekiti Kikove!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgOXyWdWR-J6O5yJoWdcU0qo_zc53qnY67FBgzk4SEqBhFStSczsNjyuN3rezbxjkOuKXigK8Q4Zv9vlu5qsyKG4u78P1GEPSdozSpbzbDFuSnnE958IIzLzipTcOLjI8JILklXULtH8EI/s1600/kikove.jpg

 
 Mwenyekiti wa YUNA Taifa Benedict Faustine Kikove


Kuna hali ya vuta nikuvute kati Mwenyekiti wa Yuna Chuo Kikuu Mzumbe Bw Jacob Julius dhidi ya Rais wa YUNA Taifa Bw Benedict Kikove Blog hii ina taarifa kamili......
Habari za uhakika ambazo zimetufikia katika chumba cha habari zinafichua hali hiyo ya kukosa maelewano baina ya viongozi hao wawili hali inayodaiwa kuchochewa na lawama za baadhi ya wanachama wa YUNA Mzumbe kutupa lawama zao kwa viongozi wa YUNA chuoni hapa kuwa ni watu "wasiowajibika" kiasi kwamba hawajafanya hata "event" moja.
Kufatia lawama hizi Blog hii iliamua kumtafuta Bw Jacob kupitia simu yake ya kiganjani ambapo alitupa lawama zake kwa uongozi wa YUNA wa Taifa kuwa hauwajibiki ipasavyo huku akisisitiza kuwa Bw Kikove anakwenda kwa "mwendo wa kobe" kwa madai kuwa anachelewa kutoa kile alichoita "GO AHEAD" kwa YUNA Mzumbe kufanya events mbalimbali.
Katika kujibu tuhuma hizo Bw Kikove kupitia simu yake ya kiganjani amenukuliwa akisema kuwa" hakuna ukweli juu ya hayo, si kweli kuwa tunawazuia wanachama wa Mzumbe kufanya events bali tunachohitaji ni informations" akaendelea kudai kuwa " ni vema hao viongozi wa YUNA Mzumbe wakaacha lawama na badala yake kila mmpja awajibike"
Bw Kikove aliendelea kusisitiza kuwa uchaguzi mkuu wa YUNA unakuja hivyo watu wajiandae kupiga kura na pia amekanusha vikali kung'ang'ania madaraka kama inavyodaiwa na baadhi ya wanachama na badala yake akasema kuwa uchaguzi ungepaswa ufanyike mwezi wa tano mwaka huu lakini ni wanachama wenyewe waliomba uahirishwe hivyo kufanyika mwezi wa tisa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment