Tuesday, September 20, 2011

Ukata Wa Fedha Za Kujikimu Wawatesa Wanamzumbe

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgQrAyngpeGxufutad2pzYgvtACNJQskFu1_Gd1YFvo5rpUi-QXGaSx1MOwH-8GDhGNh9Kwy48qTV_AkS24YrR_w-wq0UUacfCB8FBs2YGCuZtoJVid19ydWBzNanKtHMp03jI7v7iGW2aw/s1600/Noti+mpya+2011.jpgNa Riporter Wetu,
Wanafunzi wa mwaka wa kwanza walioko Stargard semister chuoni Mzumbe "hawana fedha za kujikimu" Blog hii inaripoti bila wasiwasi........
Uchunguzi uliobeba sura ya "kikachero" ulioendeshwa na jopo la waandishi wa Blog hii kwa siku nne mfululizo umeibuka na taarifa ya kusikitisha ya wanafunzi "kuishiwa hela za kujikimu maarufu kama Boom" huku ikiwa bado siku nyingi kabla ya tarehe ya kufunga chuo.
Wanafunzi wengi waliohojiwa na Blog hii wamekiri wazi "KUFULIA VIBAYA" huku wakitoa wito wa Rais wa MUSO Mh Uswege Isaac kuwaombea kwa utawala wa chuo ili waweze kukopeshwa.
Mmoja wa wanafunzi waliohojiwa na Blog hii amekaririwa akisema " aisee watu wamefulia vibaya, wewe nenda pale CRDB Bank uone kama kuna mtu anasogelea zile ATM machine pale?"
Taarifa zaidi zinabainisha sababu za kufulia huko kuwa ni pamoja na pesa hizo za boom kuingizwa kabla ya chuo kufunguliwa.
Sababu nyingine inayotajwa kuchangia hali hiyo ni pamoja na matumizi mabaya ya baadhi ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza. Uchunguzi wetu pia umebaini kuibuka kwa kasi kwa tabia ya "KUKOPANA HOVYO" miongoni mwa wanachuo kufatia hali hiyo. Mmoja wa viongozi wa dini aliyezungumza na Blog kwa sharti la kutotajwa jina ameonya kuwa iwapo hali hiyo itaachwa iendelee ipo hatari ya wanachuo hao kuporomoka kitaalamu kwasababu ya kutumia muda mwingi kuwaza wataishije chuoni hapo.
Naye mmoja wa viongozi wastaafu wa MUSO amekaririwa akisema " hili ni fundisho kwani mama Dean hakuwahi kuwaonya? nasikia si aliwaambia mwanzo wa semister mweke Bill za msosi?"



No comments:

Post a Comment