Jengo la Faculty of law linavyoonekana kwa nje(picha ya maktaba)
Na Mwandishi Wetu Morogoro Mjini,
Habari zilizotufikia hivi punde zinabainisha kuwa mwanafunzi wa Laws wa CHUO KIKUU MZUMBE jina tunalihifadhi amepata matatizo ya akili ambayo yanadaiwa kusababishwa na msongo wa mawazo .
Habari zaidi zinaeleza kuwa jamaa huyo amehitimu Mzumbe Mbeya Branch degree ya sheria mwezi wa 7 mwaka huu lakini tangu amalize hajapata ripoti yake. Jamaa huyo anadaiwa kuhamia hapa Mzumbe ambapo alikuwa akikaa kikenge kimojawapo nyuma ya Library , Blog hii imefanikiwa kuona mlango uliovunjwa na jamaa huyo kutokana na kupatwa na tatizo la akili, mpaka tunakwenda mtamboni leo hii jamaa huyo yupo hospitali ya Rufaa Morogoro Mjini.
BLOG HII INATOA POLE KWA MWANAMZUMBE HUYO NA KUMTAKIA AFYA NJEMA!
hii si nzuri sana, kungekuwa na namna ya kusaidia wanafunzi ku himili msongo wa mawazo. Hii inawezekana kama wao wanafunzi wakawatumia vizuri wasaidizi wa masuala ya kitaaluma na hata walimu wenyewe wanaowasimamia hao wanafunzi wangeweza kuwashauri wawaone hao washauri pale wanapoona mienendo ya wawasimamiao haiko vizuri,,
ReplyDelete