Tuesday, September 20, 2011

HOTUBA YA WAZIRI MKUU YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012. BUNGENI TAR. 22/08/2011.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYmsa8PsNLMu4HXEuPd5xxuAKhI7vmkXHtra5tGqf3u_52k-YCq_Cpp-1qlkZiDVeCtHboLBAAk-21VEKy39-AATr2sne1IiRLIu5psMwX31_3jGBbhrrNjePCxy59xnGQv3t9yZXwmWI/s1600/PM.jpg
 Waziri Mkuu Wa MUSO Mh Benson Futte wakwanza kushoto


Mheshimiwa. Spika,

Mheshimiwa Katibu Mkuu wa bunge,
Mheshimiwa Kaimu katibu Mkuu wa Selikari,
Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Waziri,
Waheshimiwa wabunge mabibi na mabwana Habari za wakati huu.
UTANGULIZI
Awali ya yote nitangulize shukrani za dhati kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha sote tuliopo hapa kukutana mahali hapa leo hii katika hali tulizonazo. Pili nifadhirike kwa kuwa shukuru wale wote waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali kuja kuhudhulia kikao hiki cha bunge kwa dhamana zao mbalimbali.
Pia kwa nafasi ya pekee kabisa niwashukuru waheshimiwa wabunge kwa kukubali kwenu kuahirisha shughuli zenu za masomo kwa muda hata kuitikia wito wa kikao hiki hata kukipa kipau mbele katika shughuli zenu za leo. Hakuna asiyetambua ufinyu wa muda kimasomo katika muhula huu lakini na amini yote ni moyo wa uzalendo mlionao lakini pia kujitambua nafasi na hadhi mliyo nayo katika kuwawakilisha wenzetu. Natoa msisitizo huu kwa sasbabu itakumbukwa kuwa kikao hiki cha bunge la bajeti si mara ya kwanza kukaa, mara ya kwanza ilikuwa ni tarehe 27/5/2011 lakini kwa kutokukamilika kwa idadi ya wabunge waliohitajika kuijadili bajeti bunge lile liliahilishwa ili kuilinda katiba.
Mh. Spika, hili ni bunge la bajeti. Sitasahau tulipoianza safari hii ya uongozi na sitaacha kusimulia kila inapo nilazimu kufanya hivo, kama sehemu ya mifano hai na ulinganifu wa hatua za maendeleo kwa kadili wakati unapo pita.
Mh. Spika, tumeingia kwenye serikali tukiwa tunachangamoto(kero) nyingi ukilinganisha na faraja tulizokuwa tukipata, kwa kuzitaja hizi ni baadhi tu. Mfumuko wa bei za vyakula, maswali juu ya MUSO Bar, kero za giza lililokuwa limekithili katika maeneo yetu hata kutishia usalama wetu wakati wa usiku hata watu kwa shida walizokuwa wakikabiliana nazo kufikia kusema sisi kama MUSO tutumie pesa zetu kuweka security lights katika maeneo mbalimbali ya chuo pesa abayo kiuhalisia hatukuwa nayo na hatuna, ufyekaji wa nyasi, kukithili kwa mbu, shida ya maji, ofisi za MUSO, shida ya makazi, afya pia tatizo la kutokuwa na pesa tasilimu kama selikari ya wanafunzi.
Mh. Spika, kwakuwa wakati ni kielelezo tosha cha taswira ya maendeleo tulikotoka , tulipo na tuendako, sasa wakati umefika wakuwa na uwezo wakusema selikari ipo hai na ipo kazini wakati wote kama kiungo muhimu katika kushirikiana na utawala wa chuo kutatua kero zinazo ikabili jamii yetu. Na hivo basi, pasipo kubezwa tunaweza kuanza kujivunia mafanikio yaliyoanza kupatikana kwa muda mfupi ndani ya nusu ya kwanza ya kipindi cha uongozi wa selikari hii.
Mh. Spika, Wakati umefika sasa kuruhusu matokeo ya matendo yaseme na maneno yabaki kwenye kumbukumbu kama mipango iliyozaa haya yanayoonekana. Sirahisi kulidhisha kila mmoja wetu bali nirahisi kuridhisha walio wengi kwani tuna mahitaji tofauti kwa nyakati tofauti, huku tuyaitayo mafanikio huja kwa mipango madhubuti, vipaumbele mahususi kwa wakati sahihi. Katika hili sihitaji kusimulia bali kutaja tu kwani vinaonekana na vina jieleza vyenyewe (les ipsa loquitur).
Mh. Spika, hii niorodha ndogo tu ya vitu vilivyo fuatiliwa na kufanyika baadhi vikiwa vimekamilika navingine vikiwa katika hatua mbalimbali kuelekea ukamilifu wake na hivo kwa selikari kuwa ni hatua muhimu kutoka kero hadi mafanikio: security lights zimewekwa kutoka geti kuu la kuingilia chuoni maeneo mbalimbali ya chuo hadi geti la kutokea Changarewe, upanuzi wa ofisi ya MUSO; vikenge viwili vilitengwa na sasa vipo katika hatua za mwisho za ukarabati ili tukabidhiwe, kushushwa kwa bei za vyakula katika cafeteria yetu ya Faith, kupambana na tatizo lililosumbua sana la ufyekaji wa nyasi, kukabiliana na mbu waliokuwa wamekithiri(fumigation ilifanyika),MUSO Bar ipo kwenye ukarabati, ufumbuzi wa tatizo la maji suluhisho la kudumu limepatikana; utawala umeshatenga fedha kwaajili ya kuyavuta maji kutoka kwenye kisima ambacho kilichimbwa na DDA Rwegalulia, ushiriki wa MUSO katika upangaji makazi ya wanafunzi umekubalika, habari za afya; mengi yanaendelea kufanyika ikiwa na uwepo mpango madhubuti wa bima ya afya, tulifanikiwa kufanikisha kongamano juu ya maswala mbalimbali ya A. Mashariki Tar.25 June 2011 kama moja ya madhumuni ya uwepo wa MUSO kama umoja wa wanafunzi kikatiba. Katika haya yote na mengine ambayo hayaja tajwa selikari itakuwa haina fadhira ikiwa haita ushukuru utawala wa chuo kwa mchango wao mkubwa na kukiri wazi kuwa katika vyuo vya Umma Tanzania utawala wa chuo kikuu Mzumbe ni msikivu natuitumie fursa hiyo vizuri, kwani tunapo omba jambo likashindwa kutekelezeka haimaanishi kuwa wamepuuzia bali kwa wakati huo huwa wamezidiwa uwezo wa kifedha na majukumu yanayo kikabili chuo. Hili linathibitishwa na yalioyofanyika ndani ya muda mfupi.
Mh. Spika, pamoja na hayo yote bado tunakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kuchelewa kwa mikopo kwa loan beneficiaries na hivo kudhoofisha ufanisi kwa wahanga na wakati mwingine kuigharimu selikari fedha nyingi katika kulishughulikia hili, kero za udahili kwa wenzetu wa cheti kujiunga na shahada, kero za ulevi kupita kiasi hata kutishia usalama wawengine nyakati za usiku na wengine kujikuta wapo polisi, changamoto ya uchache wavyumba vya madarasa na mabweni lakini pia hali isiyo ridhisha ya mabweni yetu tunayokaa na kwa upande wa uendeshaji wa selikari changamoto kubwa ikiwa ni ufinyu wa bajeti. Hizi ni chache tu kati ya nyingi tunazokabiliana nazo. Lakini kwa kuwa selikari haipo likizo ufumbuzi bado unatafutwa.
Mh. Spika, ukifuatilia hotuba hii kwa umakini utagundua kuwa mengi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika yamekuwa ni ya kiufuatiliaji zaidi kwa upande wa selikari na utawala ndio umekuwa ukiyagharamia, hiyo haimaanishi kwamba selikari haina ya kuyagharamia. Selikari inayo mengi ya kugharamia kwa maslahi ya wana MUSO ukilinganisha kwamba kuingia madarakani kwa selikari hii ilikuwa ni ushawishi uliotokana na sera ama ahadi za ninini selikari ingekifana ikiwa ingepata nafasi ya kuongoza kupitia kwa kiongozi mkuu wa selikari Mh Rais Uswege Isaac. Watu wakashawishika hata kuthubutu kuipa nafasi hiyo sasa wanasubili utekelezaji.
Mh. Spika, kwa kutambua umuhimu wa kutekeleza ahadi, selikari imeona haja ya kuja mbele ya bunge lako tukufu na mipango ambayo imeambatana na bajeti ya kufanikisha mipango hiyo, kwani ni ukweli usiopingika kwamba kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa kwako. Selikari kupitia kwa waziri wa fedha imeona haja ya kuleta kwenu wabunge, mapitio na muelekeo wa kazi za selikari kwa mwaka wa fedha ulioanza july 2011/2012 pia makadilio ya mapato na matumizi wakati huo wote.
Mh. Spika, selikari inaliomba bunge lako tukufu kwa utashi lililojaaliwa kuwa nao, kuipitia kiuangalifu bajeti hii na kuipitisha ilikuipa selikali nafasi na kifungo cha kwenda kutimiza yale yaliyo azimiwa, kwani hayo ndiyo yaliyo wafanya wasomi wa chuo kikuu Mzumbe kushawishika, hata kumpa Mh. Rais bwana Uswege Isaac imani na nafasi ya kuiongoza selikari yao kwa dira waliyoshawishika nayo kuwa itawafikisha kwenye hatua nyingine.
Mh. Spika, naomba pia nitumie fursa hii kuwaasa waheshimiwa wabunge kuwa watulivu huku wakijenga hoja za kujenga selikari yetu ipige hatua lakini pia wapambanue sumu zitakazopandikizwa na baadhi ya wabunge kwa kificho cha kusimamia ukweli na uhalisia. Sisi kama wasomi tusipayuke pasipo hoja ilimradi tu tusikike tukizungumza huku tukipoteza wakati ambao hatutaweza kuupata tena. Tusizungumze kwa hisia zisizo na uhalisia ilimradi tu kutimiza maslahi yetu binafsi kwa kificho cha maslahi ya umma bali tuzungumze na tujenge hoja kwa ushahidi. Tuwe kama samaki aliye hai na sio mfu.
Mh. Spika, kwa kuwa sio rahisi kuwadanganya watu wote wakati wote bali watu wote wakati fulani na watu fulani wakati wote, na wasihi msithubutu kudanganya kivuli hicho cha uwongo kisije kutufuata milele na tukawa wafu mbele ya walimwengu. Lakini pia usiwe miongoni mwa watu wakudanganywa wakati wote hata kuwa sawa na samaki mfu hata kupoteza hadhi katika nyadhifa nyingine muhimu huko maishani. Remember unspoken word never does harm.
Mh. Spika, baada ya maelezo haya kwa muhutasali naomba bunge lako liidhinishe makadilio na matumizi ya fedha kwa matumizi ya shughuli mbalimbali za selikari katika mwaka wa fedha 2011/2012 kama itakavyo wasilishwa na waziri wa fedha kwa kadili atakapopata nafasi.
Mh. Spika, pamoja na bajeti hizo zitakazosomwa kwenu hivi punde na omba niwaalike wah. Wabunge, kuendelea kutoa ushauri kwa yale wanayoona yapo kwa maslahi ya wananchi kwani sote lengo letu ni moja kujenga MUSO endelevu kwa maslahi ya vizazi vyote.
Mh. Spika, naomba kutoa hoja.

No comments:

Post a Comment