Tuesday, September 13, 2011

Mrejesho Wa Makala Inayolalamikiwai; Vita Ya Kumrithi Uswege Sasa Yapamba Moto, Kampeni Zaanza Kimyakimya!, Wenye Hoja Leteni Sasa

Rais wa sasa wa MUSO Mh Uswege Isaac

Kutokana na watu wengi kurusha shutuma kali dhidi ya habari hii wakidai imewagusa na kuwachafua baadhi ya watu Blog hii imeamua kuichapa tena habari hii ili Wanamzumbe wengi zaidi waweze kuisoma lakini si hayo tu bali pia kutoa nafasi kwa wakosoaji ili waweze kukosoa vizuri na watu wapime hoja zao kwenye mlingano wa mizania, kwa wale wenye mawazo tofauti wanaweza kutuma maoni yao kwenda musolink22@gmail.com , nasi tutayachapa bila upendeleo..................

Vita Ya Kumrithi Uswege Sasa Yapamba Moto, Kampeni Zaanza Kimyakimya !



Kuna vita ya madaraka imeanza kuelekea uchaguzi mkuu wa MUSO mwakani Blog hii inaripoti bila wasi......

Utafiti wa kina ulioendeshwa na jopo la wanahabari wa Blog hii umebainisha kuwepo kwa kampeni za chini kwa chini za baadhi ya "watu" kuwania urais.
Haijafahamika mara moja iwapo watu hao wanafahamu kuwa wanafanya makosa kuanza kampeni kabla ya muda? taarifa zaidi zinaeleza kuna mikakati mitano inayotumika kufanikisha mbinu hizo;
Kwanza ni "kujichanganya na watu" mbinu hii inafanywa kwa baadhi ya watu wenye nia ya kuwania kujisogeza karibu na watu hususani sehemu ya kula, mbinu ya pili kuvaa vizuri "kulipuka" watu hao wanadaiwa kushona nguo nzuri kiasi kwamba wanataka kujenga picha kuwa wanafaa kukabidhiwa mikoba ya Uswege, mbinu ya tatu ni socialization hawa wanatumia vitu kama mechi za kirafiki kueneza propaganda zao, nne ni kuunda mitandao ya kuratibu kampeni na tano kutumia silaha ya ufaculty.
Uchunguzi zaidi unawataja wahusika wa mbinu hizi kwa faculty zao(majina tunayahifadhi lakini baadae tutayaanika) , wahusika hao ni pamoja na yule wa social science ambaye huongea kwa upole sana na ni smart kwa mavazi kupindukia, wa pili ni yule wa Laws ambaye ni mcheshi na mwongeaji sana , wa tatu ni yule wa BPA/SOPAM ambaye anapenda kushiriki kwenye midahalo ya hapa na pale na wa nne ni yule wa Commerce ambaye anajenga nertwork yake kimyakimya kwa kushirikisha baadhi ya watu maarufu hapa chuoni.

Blog hii inatoa wito kwa wahusika kuacha vitendo hivyo kwani siyo muda muafaka hivyo ni kinyume cha sheria.




No comments:

Post a Comment