Tuesday, September 20, 2011

Wafahamu Wakuu Wapya Wa Mikoa Walioteuliwa na Rais Kikwete

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/09/dogojk4.jpg
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotolewa Dar es Salaam hivi karibuni iliwataja wakuu hao wa wilaya waliopandishwa vyeo na mikoa yao katika mabano kuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, John Tupa (Mara), DC wa Morogoro, Saidi Mwambungu (Ruvuma), Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa (Tanga), DC wa Ilala, Leonidas Gama (Kilimanjaro), DC wa Newala, Dk Rehema Nchimbi (Dodoma), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Elaston Mbwillo (Manyara).

Wengine ni DC wa Karagwe, Kanali Fabian Massawe (Kagera), DC wa Mvomero, Fatma Mwassa (Tabora), DC wa Manyoni, Ali Rufunga (Lindi), DC wa Kilombero, Mhandisi Ernest Ndikillo (Mwanza), DC wa Bagamoyo, Magesa Mulongo (Arusha). Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Stella Manyanya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Katika uteuzi huo, Mahiza anakwenda Mkoa wa Pwani, Bendera ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mwananzila Shinyanga. Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Mahiza alikuwa ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Mwananzila huku Bendera akiwa ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.

Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza, Said Mecky Sadiki anayehamia Dar es Salaam akitokea Lindi, Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma, Luteni Kanali Issa Machibya kutoka Morogoro kwenda Kigoma na Kanali Joseph Simbakalia anakwenda Mtwara akitokea Kigoma.

Wakuu wa mikoa waliostaafu ni Mohammed Babu aliyekuwa Kagera; Isidore Shirima (Arusha), Kanali Anatory Tarimo (Mtwara), John Mwakipesile (Mbeya), Kanali Enos Mfuru (Mara), Brigedia Jenerali Dk Johanes Balele (Shinyanga) na Meja Jenerali Said Kalembo (Tanga).

Wakuu wa wanne wa mikoa waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Amina Mrisho aliyekuwa Pwani, Dk James Msekela aliyekuwa Dodoma, Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Daniel Ole Njoolay wa Rukwa.

Taarifa hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu imesema: “Wakuu wa mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.”

No comments:

Post a Comment