Rais wa MUSO Mh Uswege Isaac
Minong'ono imetanda hivi punde hapa chuoni Mzumbe kutokana na kile kinachodaiwa "KUTOELEWEKA" kwa kauli ya rais wa MUSO Mh Uswege Isaac anayodaiwa kuitoa kwenye moja ya vikao vya shirikisho la vyuo vikuu Tanzania TAHILISO.
Juhudi za Blog zimefanikiwa kunasa mchango huo unaodaiwa kutolewa na Mh Uswege unasomeka hivi "
Mzumbe University Students Organisation president Uswege Isaac said he was “impressed with the way the government has responded to years of appeals by students”, but also called on university authorities to keep the prices of basic needs at current levels. He similarly called for “equally favourable consideration in the future since life is getting more and more costly every passing day”, noting that the allowance package was exclusive of public transport “for which we are paying through the nose”."
Ujumbe huu umelalamikiwa la baadhi ya wanamzumbe na unadaiwa kuibuliwa na mwanafunzi mmoja aliyekuwa mbele ya hostel ya Milambo jioni hii ambaye alidai kuwa ana uhakika kuwa Mh Uswege ameunga mkono maamuzi ya serikali ya kuongeza 7,500 badala ya elfu 10,000 kama madai ya wanafunzi kote Tanzania.
Ndipo Blog hii ilipofanya juhudi za kufa na kupona za kuunasa ujumbe huo ambao unadaiwa kutolewa na Mh Uswege.
Hata hivyo mmoja wa viongozi aliyehojiwa na Blog hii kuhusiana na sakata hilo hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kudai "UCHOCHEZI MTUPU"
No comments:
Post a Comment