(Tatizo la Maji likomeshwe haraka , linatuathiri sana HALIKUBALIKI HATA KIDOGO)
(Mh Uswege na Futte please tunataka maji ya uhakika)
Mimi kama mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe naomba kujitokeza kwenye Blog hii kutoa kilio changu kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe wakiongozwa na rais Mh Uswege Isaac.Siamini na sitaki kuamini kuwa kuna ubaguzi miongoni mwa Hostel hapa chuoni, hivi Mh Uswege na serikali yako mnaweza kutwambia kwanini tunaoishi kwenye Hostel ya KINJE hatupati maji? tena sisi ni "WASICHANA" hivi ni nini chanzo cha tatizo hili?
Si hayo tu wakati mwingine umeme unakatika hovyo, kwakweli hili HALIKUBALIKI.
Tunataka maelezo kamili kutoka MUSO ili tujue ni lini sisi wana kinje tutacha kudhurura na ndoo zetu tukiganga kusaka maji.
Nawasilisha,
Ni Mimi Mkereketwa kutoka KINJE.
No comments:
Post a Comment