Tuesday, September 20, 2011

Je Wewe Ni Mbunifu Na Mchapa Kazi? Nafasi Yako Ni Hii;The U8:Connecting Students Around the World


http://www.hillcrestumc.org/wp-content/uploads/2010/06/people-holding-hands-sunset.jpg
Mdau habari!


Kwanza hongera sana kwa initiative ya blog kuhusu wanajamii wa Mzumbe hapo.

Kifupi naitaji msaada wako kuweza kupata mwanafuzi mmoja (hardworking) kutoka katika kila chuo hapa Tanzania,ili aweze kutusaidia kupata members wa kujiunga na ummoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu duniani (The U8) amabao makao yake makuu yako UK,ni nafasi nzuri sana ya wanafunzi kuweza kuconnect na vyuo mbalimbali duniani na kuhuzuli apia mikutano y akimataifa.
Naomba soma kiambatanisho hapo juu kwa maelezo zaidi kuhusu U8 na pia nijulishe utayali wako wa kushirikiana nami katika hili.
Regards,

ORESTES SOTTA
MANAGING DIRECTOR
SOTTA&PARTNERS CONSULTING LTD
P.O.BOX 494,MOROGORO,TANZANIA EAST AFRICA.
PHONE:+255 (0) 653 07 59 49
HEAD OFFICE LOCATION-RYMA RYM BUILDING NKOMO STRT.



Jacob Julius Jaju; Sitambui Kufukuzwa Kwangu, Najitambua Kama Waziri Halali, Nataka Posho Zangu!

 
Katika hali isiyo ya kawaida Bw Jacob Julius ameibuka na kudai kuwa hatambui kile kinachoitwa "KUTEMWA UWAZIRI WA ITIFAKI"
Akizungumza na Blog hii kwa njia ya simu huku akionyesha kujiamini Jacob amekaririwa akisema " sijawahi kupewa barua ya kufukuzwa, hivyo najua mimi bado waziri wa MUSO na nitadai posho zangu"amekaririwa.
Matamshi haya ya Bw Jacob yanakuja week kadhaa baada ya Rais wa MUSO kutangaza kumtimua kazi rasmi kwa kkile kilichodaiwa kupingana na serikali yake anayotumikia.
Nao upande wa serikali ya MUSO kupitia kwa katibu wa wizara ya Itifaki Bw Raymond Kyara umesema kuwa ni kweli Bw Jacob alifutwa uwaziri lakini hata yeye amekiri kutofahamu iwapo Jacob alipewa barua au la.
Iwapo ni kweli anayodai Bw Jacob basi kuna hatari kubwa ya hatua hii ya kutopewa rasmi barua ya kufukuzwa ikakuza mjadala huo na kuleta utata mkubwa.
Aki

Ukata Wa Fedha Za Kujikimu Wawatesa Wanamzumbe

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgQrAyngpeGxufutad2pzYgvtACNJQskFu1_Gd1YFvo5rpUi-QXGaSx1MOwH-8GDhGNh9Kwy48qTV_AkS24YrR_w-wq0UUacfCB8FBs2YGCuZtoJVid19ydWBzNanKtHMp03jI7v7iGW2aw/s1600/Noti+mpya+2011.jpgNa Riporter Wetu,
Wanafunzi wa mwaka wa kwanza walioko Stargard semister chuoni Mzumbe "hawana fedha za kujikimu" Blog hii inaripoti bila wasiwasi........
Uchunguzi uliobeba sura ya "kikachero" ulioendeshwa na jopo la waandishi wa Blog hii kwa siku nne mfululizo umeibuka na taarifa ya kusikitisha ya wanafunzi "kuishiwa hela za kujikimu maarufu kama Boom" huku ikiwa bado siku nyingi kabla ya tarehe ya kufunga chuo.
Wanafunzi wengi waliohojiwa na Blog hii wamekiri wazi "KUFULIA VIBAYA" huku wakitoa wito wa Rais wa MUSO Mh Uswege Isaac kuwaombea kwa utawala wa chuo ili waweze kukopeshwa.
Mmoja wa wanafunzi waliohojiwa na Blog hii amekaririwa akisema " aisee watu wamefulia vibaya, wewe nenda pale CRDB Bank uone kama kuna mtu anasogelea zile ATM machine pale?"
Taarifa zaidi zinabainisha sababu za kufulia huko kuwa ni pamoja na pesa hizo za boom kuingizwa kabla ya chuo kufunguliwa.
Sababu nyingine inayotajwa kuchangia hali hiyo ni pamoja na matumizi mabaya ya baadhi ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza. Uchunguzi wetu pia umebaini kuibuka kwa kasi kwa tabia ya "KUKOPANA HOVYO" miongoni mwa wanachuo kufatia hali hiyo. Mmoja wa viongozi wa dini aliyezungumza na Blog kwa sharti la kutotajwa jina ameonya kuwa iwapo hali hiyo itaachwa iendelee ipo hatari ya wanachuo hao kuporomoka kitaalamu kwasababu ya kutumia muda mwingi kuwaza wataishije chuoni hapo.
Naye mmoja wa viongozi wastaafu wa MUSO amekaririwa akisema " hili ni fundisho kwani mama Dean hakuwahi kuwaonya? nasikia si aliwaambia mwanzo wa semister mweke Bill za msosi?"



HOTUBA YA WAZIRI MKUU YA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012. BUNGENI TAR. 22/08/2011.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYmsa8PsNLMu4HXEuPd5xxuAKhI7vmkXHtra5tGqf3u_52k-YCq_Cpp-1qlkZiDVeCtHboLBAAk-21VEKy39-AATr2sne1IiRLIu5psMwX31_3jGBbhrrNjePCxy59xnGQv3t9yZXwmWI/s1600/PM.jpg
 Waziri Mkuu Wa MUSO Mh Benson Futte wakwanza kushoto


Mheshimiwa. Spika,

Mheshimiwa Katibu Mkuu wa bunge,
Mheshimiwa Kaimu katibu Mkuu wa Selikari,
Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Waziri,
Waheshimiwa wabunge mabibi na mabwana Habari za wakati huu.
UTANGULIZI
Awali ya yote nitangulize shukrani za dhati kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha sote tuliopo hapa kukutana mahali hapa leo hii katika hali tulizonazo. Pili nifadhirike kwa kuwa shukuru wale wote waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali kuja kuhudhulia kikao hiki cha bunge kwa dhamana zao mbalimbali.
Pia kwa nafasi ya pekee kabisa niwashukuru waheshimiwa wabunge kwa kukubali kwenu kuahirisha shughuli zenu za masomo kwa muda hata kuitikia wito wa kikao hiki hata kukipa kipau mbele katika shughuli zenu za leo. Hakuna asiyetambua ufinyu wa muda kimasomo katika muhula huu lakini na amini yote ni moyo wa uzalendo mlionao lakini pia kujitambua nafasi na hadhi mliyo nayo katika kuwawakilisha wenzetu. Natoa msisitizo huu kwa sasbabu itakumbukwa kuwa kikao hiki cha bunge la bajeti si mara ya kwanza kukaa, mara ya kwanza ilikuwa ni tarehe 27/5/2011 lakini kwa kutokukamilika kwa idadi ya wabunge waliohitajika kuijadili bajeti bunge lile liliahilishwa ili kuilinda katiba.
Mh. Spika, hili ni bunge la bajeti. Sitasahau tulipoianza safari hii ya uongozi na sitaacha kusimulia kila inapo nilazimu kufanya hivo, kama sehemu ya mifano hai na ulinganifu wa hatua za maendeleo kwa kadili wakati unapo pita.
Mh. Spika, tumeingia kwenye serikali tukiwa tunachangamoto(kero) nyingi ukilinganisha na faraja tulizokuwa tukipata, kwa kuzitaja hizi ni baadhi tu. Mfumuko wa bei za vyakula, maswali juu ya MUSO Bar, kero za giza lililokuwa limekithili katika maeneo yetu hata kutishia usalama wetu wakati wa usiku hata watu kwa shida walizokuwa wakikabiliana nazo kufikia kusema sisi kama MUSO tutumie pesa zetu kuweka security lights katika maeneo mbalimbali ya chuo pesa abayo kiuhalisia hatukuwa nayo na hatuna, ufyekaji wa nyasi, kukithili kwa mbu, shida ya maji, ofisi za MUSO, shida ya makazi, afya pia tatizo la kutokuwa na pesa tasilimu kama selikari ya wanafunzi.
Mh. Spika, kwakuwa wakati ni kielelezo tosha cha taswira ya maendeleo tulikotoka , tulipo na tuendako, sasa wakati umefika wakuwa na uwezo wakusema selikari ipo hai na ipo kazini wakati wote kama kiungo muhimu katika kushirikiana na utawala wa chuo kutatua kero zinazo ikabili jamii yetu. Na hivo basi, pasipo kubezwa tunaweza kuanza kujivunia mafanikio yaliyoanza kupatikana kwa muda mfupi ndani ya nusu ya kwanza ya kipindi cha uongozi wa selikari hii.
Mh. Spika, Wakati umefika sasa kuruhusu matokeo ya matendo yaseme na maneno yabaki kwenye kumbukumbu kama mipango iliyozaa haya yanayoonekana. Sirahisi kulidhisha kila mmoja wetu bali nirahisi kuridhisha walio wengi kwani tuna mahitaji tofauti kwa nyakati tofauti, huku tuyaitayo mafanikio huja kwa mipango madhubuti, vipaumbele mahususi kwa wakati sahihi. Katika hili sihitaji kusimulia bali kutaja tu kwani vinaonekana na vina jieleza vyenyewe (les ipsa loquitur).
Mh. Spika, hii niorodha ndogo tu ya vitu vilivyo fuatiliwa na kufanyika baadhi vikiwa vimekamilika navingine vikiwa katika hatua mbalimbali kuelekea ukamilifu wake na hivo kwa selikari kuwa ni hatua muhimu kutoka kero hadi mafanikio: security lights zimewekwa kutoka geti kuu la kuingilia chuoni maeneo mbalimbali ya chuo hadi geti la kutokea Changarewe, upanuzi wa ofisi ya MUSO; vikenge viwili vilitengwa na sasa vipo katika hatua za mwisho za ukarabati ili tukabidhiwe, kushushwa kwa bei za vyakula katika cafeteria yetu ya Faith, kupambana na tatizo lililosumbua sana la ufyekaji wa nyasi, kukabiliana na mbu waliokuwa wamekithiri(fumigation ilifanyika),MUSO Bar ipo kwenye ukarabati, ufumbuzi wa tatizo la maji suluhisho la kudumu limepatikana; utawala umeshatenga fedha kwaajili ya kuyavuta maji kutoka kwenye kisima ambacho kilichimbwa na DDA Rwegalulia, ushiriki wa MUSO katika upangaji makazi ya wanafunzi umekubalika, habari za afya; mengi yanaendelea kufanyika ikiwa na uwepo mpango madhubuti wa bima ya afya, tulifanikiwa kufanikisha kongamano juu ya maswala mbalimbali ya A. Mashariki Tar.25 June 2011 kama moja ya madhumuni ya uwepo wa MUSO kama umoja wa wanafunzi kikatiba. Katika haya yote na mengine ambayo hayaja tajwa selikari itakuwa haina fadhira ikiwa haita ushukuru utawala wa chuo kwa mchango wao mkubwa na kukiri wazi kuwa katika vyuo vya Umma Tanzania utawala wa chuo kikuu Mzumbe ni msikivu natuitumie fursa hiyo vizuri, kwani tunapo omba jambo likashindwa kutekelezeka haimaanishi kuwa wamepuuzia bali kwa wakati huo huwa wamezidiwa uwezo wa kifedha na majukumu yanayo kikabili chuo. Hili linathibitishwa na yalioyofanyika ndani ya muda mfupi.
Mh. Spika, pamoja na hayo yote bado tunakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kuchelewa kwa mikopo kwa loan beneficiaries na hivo kudhoofisha ufanisi kwa wahanga na wakati mwingine kuigharimu selikari fedha nyingi katika kulishughulikia hili, kero za udahili kwa wenzetu wa cheti kujiunga na shahada, kero za ulevi kupita kiasi hata kutishia usalama wawengine nyakati za usiku na wengine kujikuta wapo polisi, changamoto ya uchache wavyumba vya madarasa na mabweni lakini pia hali isiyo ridhisha ya mabweni yetu tunayokaa na kwa upande wa uendeshaji wa selikari changamoto kubwa ikiwa ni ufinyu wa bajeti. Hizi ni chache tu kati ya nyingi tunazokabiliana nazo. Lakini kwa kuwa selikari haipo likizo ufumbuzi bado unatafutwa.
Mh. Spika, ukifuatilia hotuba hii kwa umakini utagundua kuwa mengi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika yamekuwa ni ya kiufuatiliaji zaidi kwa upande wa selikari na utawala ndio umekuwa ukiyagharamia, hiyo haimaanishi kwamba selikari haina ya kuyagharamia. Selikari inayo mengi ya kugharamia kwa maslahi ya wana MUSO ukilinganisha kwamba kuingia madarakani kwa selikari hii ilikuwa ni ushawishi uliotokana na sera ama ahadi za ninini selikari ingekifana ikiwa ingepata nafasi ya kuongoza kupitia kwa kiongozi mkuu wa selikari Mh Rais Uswege Isaac. Watu wakashawishika hata kuthubutu kuipa nafasi hiyo sasa wanasubili utekelezaji.
Mh. Spika, kwa kutambua umuhimu wa kutekeleza ahadi, selikari imeona haja ya kuja mbele ya bunge lako tukufu na mipango ambayo imeambatana na bajeti ya kufanikisha mipango hiyo, kwani ni ukweli usiopingika kwamba kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa kwako. Selikari kupitia kwa waziri wa fedha imeona haja ya kuleta kwenu wabunge, mapitio na muelekeo wa kazi za selikari kwa mwaka wa fedha ulioanza july 2011/2012 pia makadilio ya mapato na matumizi wakati huo wote.
Mh. Spika, selikari inaliomba bunge lako tukufu kwa utashi lililojaaliwa kuwa nao, kuipitia kiuangalifu bajeti hii na kuipitisha ilikuipa selikali nafasi na kifungo cha kwenda kutimiza yale yaliyo azimiwa, kwani hayo ndiyo yaliyo wafanya wasomi wa chuo kikuu Mzumbe kushawishika, hata kumpa Mh. Rais bwana Uswege Isaac imani na nafasi ya kuiongoza selikari yao kwa dira waliyoshawishika nayo kuwa itawafikisha kwenye hatua nyingine.
Mh. Spika, naomba pia nitumie fursa hii kuwaasa waheshimiwa wabunge kuwa watulivu huku wakijenga hoja za kujenga selikari yetu ipige hatua lakini pia wapambanue sumu zitakazopandikizwa na baadhi ya wabunge kwa kificho cha kusimamia ukweli na uhalisia. Sisi kama wasomi tusipayuke pasipo hoja ilimradi tu tusikike tukizungumza huku tukipoteza wakati ambao hatutaweza kuupata tena. Tusizungumze kwa hisia zisizo na uhalisia ilimradi tu kutimiza maslahi yetu binafsi kwa kificho cha maslahi ya umma bali tuzungumze na tujenge hoja kwa ushahidi. Tuwe kama samaki aliye hai na sio mfu.
Mh. Spika, kwa kuwa sio rahisi kuwadanganya watu wote wakati wote bali watu wote wakati fulani na watu fulani wakati wote, na wasihi msithubutu kudanganya kivuli hicho cha uwongo kisije kutufuata milele na tukawa wafu mbele ya walimwengu. Lakini pia usiwe miongoni mwa watu wakudanganywa wakati wote hata kuwa sawa na samaki mfu hata kupoteza hadhi katika nyadhifa nyingine muhimu huko maishani. Remember unspoken word never does harm.
Mh. Spika, baada ya maelezo haya kwa muhutasali naomba bunge lako liidhinishe makadilio na matumizi ya fedha kwa matumizi ya shughuli mbalimbali za selikari katika mwaka wa fedha 2011/2012 kama itakavyo wasilishwa na waziri wa fedha kwa kadili atakapopata nafasi.
Mh. Spika, pamoja na bajeti hizo zitakazosomwa kwenu hivi punde na omba niwaalike wah. Wabunge, kuendelea kutoa ushauri kwa yale wanayoona yapo kwa maslahi ya wananchi kwani sote lengo letu ni moja kujenga MUSO endelevu kwa maslahi ya vizazi vyote.
Mh. Spika, naomba kutoa hoja.

Wafahamu Wakuu Wapya Wa Mikoa Walioteuliwa na Rais Kikwete

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/09/dogojk4.jpg
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotolewa Dar es Salaam hivi karibuni iliwataja wakuu hao wa wilaya waliopandishwa vyeo na mikoa yao katika mabano kuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, John Tupa (Mara), DC wa Morogoro, Saidi Mwambungu (Ruvuma), Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Chiku Gallawa (Tanga), DC wa Ilala, Leonidas Gama (Kilimanjaro), DC wa Newala, Dk Rehema Nchimbi (Dodoma), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Elaston Mbwillo (Manyara).

Wengine ni DC wa Karagwe, Kanali Fabian Massawe (Kagera), DC wa Mvomero, Fatma Mwassa (Tabora), DC wa Manyoni, Ali Rufunga (Lindi), DC wa Kilombero, Mhandisi Ernest Ndikillo (Mwanza), DC wa Bagamoyo, Magesa Mulongo (Arusha). Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Stella Manyanya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Katika uteuzi huo, Mahiza anakwenda Mkoa wa Pwani, Bendera ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mwananzila Shinyanga. Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Mahiza alikuwa ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Mwananzila huku Bendera akiwa ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.

Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza, Said Mecky Sadiki anayehamia Dar es Salaam akitokea Lindi, Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma, Luteni Kanali Issa Machibya kutoka Morogoro kwenda Kigoma na Kanali Joseph Simbakalia anakwenda Mtwara akitokea Kigoma.

Wakuu wa mikoa waliostaafu ni Mohammed Babu aliyekuwa Kagera; Isidore Shirima (Arusha), Kanali Anatory Tarimo (Mtwara), John Mwakipesile (Mbeya), Kanali Enos Mfuru (Mara), Brigedia Jenerali Dk Johanes Balele (Shinyanga) na Meja Jenerali Said Kalembo (Tanga).

Wakuu wa wanne wa mikoa waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Amina Mrisho aliyekuwa Pwani, Dk James Msekela aliyekuwa Dodoma, Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Daniel Ole Njoolay wa Rukwa.

Taarifa hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu imesema: “Wakuu wa mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.”

YUNA Mzumbe Hali Si Shwari; Jacob Atupa Lawama Kwa Mwenyekiti Kikove!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgOXyWdWR-J6O5yJoWdcU0qo_zc53qnY67FBgzk4SEqBhFStSczsNjyuN3rezbxjkOuKXigK8Q4Zv9vlu5qsyKG4u78P1GEPSdozSpbzbDFuSnnE958IIzLzipTcOLjI8JILklXULtH8EI/s1600/kikove.jpg

 
 Mwenyekiti wa YUNA Taifa Benedict Faustine Kikove


Kuna hali ya vuta nikuvute kati Mwenyekiti wa Yuna Chuo Kikuu Mzumbe Bw Jacob Julius dhidi ya Rais wa YUNA Taifa Bw Benedict Kikove Blog hii ina taarifa kamili......
Habari za uhakika ambazo zimetufikia katika chumba cha habari zinafichua hali hiyo ya kukosa maelewano baina ya viongozi hao wawili hali inayodaiwa kuchochewa na lawama za baadhi ya wanachama wa YUNA Mzumbe kutupa lawama zao kwa viongozi wa YUNA chuoni hapa kuwa ni watu "wasiowajibika" kiasi kwamba hawajafanya hata "event" moja.
Kufatia lawama hizi Blog hii iliamua kumtafuta Bw Jacob kupitia simu yake ya kiganjani ambapo alitupa lawama zake kwa uongozi wa YUNA wa Taifa kuwa hauwajibiki ipasavyo huku akisisitiza kuwa Bw Kikove anakwenda kwa "mwendo wa kobe" kwa madai kuwa anachelewa kutoa kile alichoita "GO AHEAD" kwa YUNA Mzumbe kufanya events mbalimbali.
Katika kujibu tuhuma hizo Bw Kikove kupitia simu yake ya kiganjani amenukuliwa akisema kuwa" hakuna ukweli juu ya hayo, si kweli kuwa tunawazuia wanachama wa Mzumbe kufanya events bali tunachohitaji ni informations" akaendelea kudai kuwa " ni vema hao viongozi wa YUNA Mzumbe wakaacha lawama na badala yake kila mmpja awajibike"
Bw Kikove aliendelea kusisitiza kuwa uchaguzi mkuu wa YUNA unakuja hivyo watu wajiandae kupiga kura na pia amekanusha vikali kung'ang'ania madaraka kama inavyodaiwa na baadhi ya wanachama na badala yake akasema kuwa uchaguzi ungepaswa ufanyike mwezi wa tano mwaka huu lakini ni wanachama wenyewe waliomba uahirishwe hivyo kufanyika mwezi wa tisa mwaka huu.

Wednesday, September 14, 2011

By Laws Za Banzi Kutupwa Ili Kuengua Wagombea Urais MUSO!

Taarifa za ndani zinafichua mpango wa kuwaengua baadhi ya wagombea urais MUSO mwakani kwa kutupilia mbali kile kinachoitwa "Election by-laws" zilizopitishwa wakati wa Raphael Banzi.

Taarifa kutoka kwa vyanzo vyetu vilivyo karibu na ofisi kuu ya MUSO zinatanabaisha kuwa mpango huo unasukwa mahususi ili kuwashughulikia baadhi ya wale wanaotajwa kuwa na "KIHEREHERE"

Blog hii ina taarifa za uhakika za mpango huo unaoratibiwa kwa kuwashirikisha baadhi ya wabunge ili kutengua election by laws hatua itakayopelekea kurudisha kipengele cha GPA ya 3.5 kwa wagombea urais wa MUSO hatua inayotajwa itawaengua baadhi ya watu wenye azma ya kuwania nafasi hiyo ya urais.
Hatahivyo tayari baadhi ya juhudi za kupinga mpango huo kwa kuwachochea wabunge kuugomea zimeanza huku ikidaiwa ni watu wawili wenye nia ya kugombea wanaoinjinia mpango huo.

Iwe isiwe inatosha kusema kuwa kilele cha yote haya itakuwa ni bunge lijalo la MUSO.

For Academic Centre Like Mzumbe We Need Such Views.....Read More!


John Mashaka;Our Nation Has Been Attacked , We Need A Response!



By John Mashaka,
Our nation has been befallen by a tragedy following the capsizing of MV Islander, which became a death trap to hundreds of innocent lives. Following the disaster, our head of state cut short his foreign trip to join his nation in agonizing pain, sorrow and grief. Unfortunately, while the whole country focused its attention on the tragic events in Zanzibar, our very freedom, culture, social beliefs, peace and tranquility in which many companies are banking on for their monetary gains was under assault. Our nation has been attacked from within by the hypocritical dark forces with no regard to human dignity and decency
In the midst of our lamentations, our young sisters were being paraded half naked at Mlimani City, with their images beamed into the millions of grieving households in the name of beauty pageantry. These all took place while bodies of infant children were floating lifelessly in the waters of Indian Ocean. What a shame? We have been humiliated. This should however, not come as a surprise, because after all, these companies have been in the fore-front promoting moral decay in our society by sponsoring bogus events while shrugging off real needs in health and education

Mungu Ibariki Tanzania

mashaka.john@yahoo.com

Our culture and morals have been compromised by the very companies that “hypocritically” preach social responsibility through deception and unsustainable handovers to the vulnerable as well as sponsoring pool events, and bogus tournaments at the glare of cameras. I wonder what losses would they have incurred should they have postponed the event by a week to honor the dead? Mind you, they have been running and operating this contest for months now. Miss Tanzania pageantry sponsors and organizers would have strategically gained more by being sensitive to the grieving Tanzanian public
These companies have not only insulted the Government of Tanzania, but also insulted the people of Tanzania. They have attacked both Muslims and Christians alike. They have attacked our flag that unites CCM, CUF and CHADEMA parties. They have exposed their callous nature, greed and insensitivity to life of by dining and wining yet the whole country is grieving. Some American churches with September 11th memorial celebrations at hand, devoted 30 minutes to pray for the people of Tanzania, by showing images and videos of a mourning nation. Yet companies that depend on us for their existence were insulting our morals and culture by parading young women to the victims of MV- Islander
Multinationals in our country have been operating with impunity as if they are above the law. They have constantly violated laws of the land, abused our people without anybody raising a finger at them. They have repeatedly perpetrated a cycle of violence and left many people dead. Time has come in which all these MUST STOP. Their moral compass is pointing towards a wrong direction and gone too far in their pursuit for money. It is important we remind them that, our culture values and respect the sanctity of life, and under no circumstances, can we allow them to scorn us while we mourn our dead
If these companies thought, that they could insult the government and get away with it, well, they got it wrong. They must now be reminded that, the government of the day derives its power from the people. We the people cannot let our culture and freedom be attacked. Time has come for us to stand up to these corporations and say NO. We are therefore requesting the sponsors of the beauty pageantry eight days to explain to the public as to why they insulted and attacked our cultural values. Else, we will proceed with a global call for action, which includes unspecified number of measures against them. Millions of patriots around the globe are eagerly awaiting their response under the impartial court of public justice
John Mashaka

Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma SOCIOLOGY CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) yatoa salam za Rambirambi


THE UNIVERSITY OF DODOMA SOCIOLOGY STUDENTS ORGANIZATION (UDOMSSO) 
 

Kwa niaba ya Jumuiya ya Wanafunzi Wanaosoma Shahada Ya Kwanza Ya Sosholojia (Bachelor Of Arts in Sociology) ya Chuo Kikuu Cha Dodoma   inapenda kuwapa pole watanzania wenzetu wa Tanzania Bara Na Visiwani Zanzibar kwa msiba mkubwa uliolikumba taifa

Wanafunzi tunaosoma Shahada ya Kwanza Chuo Kikuu Cha Dodoma Tunapenda Kutoa Salamu Zetu Za Rambi Rambi Kwa Raisi Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete na Raisi Wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein Kufuatia Msiba Mkubwa uliolikumba Taifa Baada Ya Kuzama Kwa Meli Ya Spice Ireland Usiku Wa Kuamkia Jumapili ambapo Mamia ya Watu waliweza Kupoteza maisha na Wengine Kujeruhiwa Na Wengiwe wakiwa hawajurikani wapi walipo mpaka sasa.
Vilevile Tunapenda Kutoa Salamu Zetu Za Rambirambi Kwa Ndugu, Jamaa Na Marafiki ambao wamepoteza Jamaa,Ndugu, Marafiki zao Katika Ajali hiyo Kubwa iliyoikumba Taifa letu

Pia tunatoa Salamu zetu Za Rambi Rambi Kwa Mwanafunzi Mwenzetu LAHYA Na Wengine Wote Walioguswa moja kwa moja Na Ajali Hii ya Meli iliyopelekea Kupoteza maisha ya Watu wengi.

Wanafunzi Wote Tunaosoma Shahada ya Kwanza Ya Sociology na Shahada Nyingine Za Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) tunaungana na Taifa kwa pamoja katika wakati huu mgumu na pia tuko tayari kushirikiana kwa hali na mali kuwafariji ndugu na jamaa kwenye msiba huu. 
 
Mungu azilaze Roho Za Marehemu Mahala Pepa Peponi Amina na Mungu Awabariki Na Kuwajaza Nguvu Ndugu, Jamaa na Marafiki Kwa Kuwapoteza Wapendwa Wao

 
 
 
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA
 

  Imetolewa Na
Josephat Lukaza
AFISA UHUSIANO 
THE UNIVERSITY OF DODOMA SOCIOLOGY STUDENTS ORGANIZATION(UDOMSSO)

Tuesday, September 13, 2011

Mrejesho Wa Makala Inayolalamikiwai; Vita Ya Kumrithi Uswege Sasa Yapamba Moto, Kampeni Zaanza Kimyakimya!, Wenye Hoja Leteni Sasa

Rais wa sasa wa MUSO Mh Uswege Isaac

Kutokana na watu wengi kurusha shutuma kali dhidi ya habari hii wakidai imewagusa na kuwachafua baadhi ya watu Blog hii imeamua kuichapa tena habari hii ili Wanamzumbe wengi zaidi waweze kuisoma lakini si hayo tu bali pia kutoa nafasi kwa wakosoaji ili waweze kukosoa vizuri na watu wapime hoja zao kwenye mlingano wa mizania, kwa wale wenye mawazo tofauti wanaweza kutuma maoni yao kwenda musolink22@gmail.com , nasi tutayachapa bila upendeleo..................

Vita Ya Kumrithi Uswege Sasa Yapamba Moto, Kampeni Zaanza Kimyakimya !



Kuna vita ya madaraka imeanza kuelekea uchaguzi mkuu wa MUSO mwakani Blog hii inaripoti bila wasi......

Utafiti wa kina ulioendeshwa na jopo la wanahabari wa Blog hii umebainisha kuwepo kwa kampeni za chini kwa chini za baadhi ya "watu" kuwania urais.
Haijafahamika mara moja iwapo watu hao wanafahamu kuwa wanafanya makosa kuanza kampeni kabla ya muda? taarifa zaidi zinaeleza kuna mikakati mitano inayotumika kufanikisha mbinu hizo;
Kwanza ni "kujichanganya na watu" mbinu hii inafanywa kwa baadhi ya watu wenye nia ya kuwania kujisogeza karibu na watu hususani sehemu ya kula, mbinu ya pili kuvaa vizuri "kulipuka" watu hao wanadaiwa kushona nguo nzuri kiasi kwamba wanataka kujenga picha kuwa wanafaa kukabidhiwa mikoba ya Uswege, mbinu ya tatu ni socialization hawa wanatumia vitu kama mechi za kirafiki kueneza propaganda zao, nne ni kuunda mitandao ya kuratibu kampeni na tano kutumia silaha ya ufaculty.
Uchunguzi zaidi unawataja wahusika wa mbinu hizi kwa faculty zao(majina tunayahifadhi lakini baadae tutayaanika) , wahusika hao ni pamoja na yule wa social science ambaye huongea kwa upole sana na ni smart kwa mavazi kupindukia, wa pili ni yule wa Laws ambaye ni mcheshi na mwongeaji sana , wa tatu ni yule wa BPA/SOPAM ambaye anapenda kushiriki kwenye midahalo ya hapa na pale na wa nne ni yule wa Commerce ambaye anajenga nertwork yake kimyakimya kwa kushirikisha baadhi ya watu maarufu hapa chuoni.

Blog hii inatoa wito kwa wahusika kuacha vitendo hivyo kwani siyo muda muafaka hivyo ni kinyume cha sheria.




Monday, September 12, 2011

Breaking Neewz! Kauli Ya Rais Wa MUSO Yazua Mtafaruku!


                Rais wa MUSO Mh Uswege Isaac
Minong'ono imetanda hivi punde hapa chuoni Mzumbe kutokana na kile kinachodaiwa "KUTOELEWEKA" kwa kauli ya rais wa MUSO Mh Uswege Isaac anayodaiwa kuitoa kwenye moja ya vikao vya shirikisho la vyuo vikuu Tanzania TAHILISO.

Juhudi za Blog zimefanikiwa kunasa mchango huo unaodaiwa kutolewa na Mh Uswege unasomeka hivi "
Mzumbe University Students Organisation president Uswege Isaac said he was “impressed with the way the government has responded to years of appeals by students”, but also called on university authorities to keep the prices of basic needs at current levels. He similarly called for “equally favourable consideration in the future since life is getting more and more costly every passing day”, noting that the allowance package was exclusive of public transport “for which we are paying through the nose”."
Ujumbe huu umelalamikiwa la baadhi ya wanamzumbe na unadaiwa kuibuliwa na mwanafunzi mmoja aliyekuwa mbele ya hostel ya Milambo jioni hii ambaye alidai kuwa ana uhakika kuwa Mh Uswege ameunga mkono maamuzi ya serikali ya kuongeza 7,500 badala ya elfu 10,000 kama madai ya wanafunzi kote Tanzania.
Ndipo Blog hii ilipofanya juhudi za kufa na kupona za kuunasa ujumbe huo ambao unadaiwa kutolewa na Mh Uswege.
Hata hivyo mmoja wa viongozi aliyehojiwa na Blog hii kuhusiana na sakata hilo hakuwa na mengi ya kusema zaidi ya kudai "UCHOCHEZI MTUPU"

Wanamzumbe 300 Kuchangia Bank ya Taifa Ya Damu!

Wanafunzi 300 wa chuo kikuu Mzumbe wamejitolea kuchangia damu kwenye bank ya damu ya taifa kuptia chama cha Red Cross Tanzania...soma habari kamili hapa.............

University students enroll to alleviate blood shor
 

Over 300 students of Mzumbe University in Morogoro have enrolled to voluntarily donate blood and help alleviate the blood shortage that has of late hit most hospitals countrywide. This was during a one-day Tanzania Red Cross Society (TRCS) mobilization and sensitization session yesterday that was held at the University.
The students̢۪ commitment comes a couple weeks after TRCS conceded reports of some unscrupulous medical workers selling blood, a development that was feared to worsen the availability of an already scarce commodity in hospitals countrywide.
TRCS as a lead government agency of blood donation mobilization in 11 regions, said measures were put in place by the ministry of health to handle the situation and deal with culprits accordingly.
â€Å“The society reported the complaint of blood selling to the ministry. We are confident that it’s playing the due role to end the vise. And we have also put up our own means to make sure that no blood including the one we are getting from Mzumbe students reaches the targeted population,”, said the Morogoro TRCS regional coordinator, Willy Mathew
Students who also enrolled as Red Cross Volunteers in the region pledged to cooperate with the society to make sure that blood shortage in the country becomes history.
â€Å“We shall work closely with TRCS to ensure that all higher learning institutions in the region are reached to not only mobilize blood donation, but also mobilize them to volunteer for the society”, students council President, Isaac Uswege said.
He added, â€Å“I and colleagues shall work hard to ensure that before the end of the month of August we have established a Red Cross Club with not less than 500 fully paid up members. And all of them must be active in this mobilization. What we need is TRCS blessing and to avail us with necessary training and relevant learning materials.
Uswege who has meanwhile volunteered to head the Red Cross club at the campus in mobilization for TRCS said students have overwhelmingly liked Red Cross and are very eager to straight away start working with the society closely.
In another development, the Mzumbe University Deputy Vice Chancellor-Administration, Prof. Faustine Kamuzora also said that he will personally donate blood as it̢۪s not his first time and to volunteer working closely with the society in mobilizing support of humanity at the campus and beyond.
â€Å“I personally cherish Red Cross commitment in response to disasters and I pledge to donate blood and also assist where I am asked for the success TRCS as an auxiliary to the government.
End.

Tatizo la Maji Mzumbe University; MUSO Mko wapi?



                (Tatizo la Maji likomeshwe haraka , linatuathiri sana HALIKUBALIKI HATA KIDOGO)
(Mh Uswege na Futte please tunataka maji ya uhakika)
Mimi kama mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe naomba kujitokeza kwenye Blog hii kutoa kilio changu kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe wakiongozwa na rais Mh Uswege Isaac.
 Siamini na sitaki kuamini kuwa kuna ubaguzi miongoni mwa Hostel hapa chuoni, hivi Mh Uswege na serikali yako mnaweza kutwambia kwanini tunaoishi kwenye Hostel ya KINJE hatupati maji? tena sisi ni "WASICHANA" hivi ni nini chanzo cha tatizo hili?
Si hayo tu wakati mwingine umeme unakatika hovyo, kwakweli hili HALIKUBALIKI.
Tunataka maelezo kamili kutoka MUSO ili tujue ni lini sisi wana kinje tutacha kudhurura na ndoo zetu tukiganga kusaka maji.

Nawasilisha,

Ni Mimi Mkereketwa kutoka KINJE.

Jamii Forums(JF) Waendelea Kumchafua Dr Mbwambo wa Mzumbe University!

Dr Mbwambo
Mtandao maarufu wa Habari wa Kijamii wa Jamii Forums maarufu kama JF unadaiwa kuendeleza msimamo wake wa kumchafua Dr Andrew Mbwambo ambaye ni Dean wa School of Business tawi la Mzumbe la jijini Dar es salaam kuwa hana PHD.

Taarifa za uhakika ambazo Blog hii inazo zinaonyesha kuwa ujumbe huo unaodaiwa kumchafua Dr Andrew Mbwambo uliopachikwa jina la "Je "Dr" Mbwambo wa Mzumbe University Dar Business School ame-graduate PhD yake?",  ujumbe huo ambao umechapwa tangu tarehe 6th April 2009  muda 19:16 p.m kwa saa za Afrika Mashariki unaendelea kudai hivi "Kwa Wadau Wote: Kwa kuwa naamini kuwa inawezekana naweza kuwa nakosea, na kuwa nimesikia au najua kupitia vyanzo mbalimbali kuwa anayejiita "DR" MBWAMBO, ambaye ni Dean wa Mzumbe University Dar Business School, hajamaliza bado PhD yake huko Nairobi University...naombeni uelewa wenu katika hili. Na kama bado, ina maana gani? na Ina picha gani kwa Mzumbe University kwa ujumla? Hili si jungu...ni utafutaji wa ukweli...

Mkereketwa! "


Haijaeleweka  mara moja lengo la mwandishi wa habari hiyo ambaye hata hivyo anatumia jina bandia la "qwerty3 ", madai haya yanaendelea kukumbatiwa na mtandao huo kwa zaidi ya miaka miwili sasa huku tukiwa na taarifa rasmi kuwa anayeitwa Dr Mbwambo ni kweli ni PHD Holder ambaye ulimwengu mzima unamtambua kuwa ni msomi mwenye kiwango hicho cha juu cha elimu yaani PHD.

Tunadhani huu ni mwanzo mzuri kwa Dr Mbwambo na Chuo Kikuu Mzumbe kulifatilia sakata hili ambalo kwa namna moja au nyingine linamchafua msomi huyo na Chuo kikuu Mzumbe.

BLOG HII INATOA POLE KWA DR MBWAMBO KWA ATHARI ZOTE ZINAZOSABABISHWA NA UZUSHI HUU NA PROPAGANDA HIZI CHAFU.

Saturday, September 10, 2011

Workshop Ya East Africa Trainers Ni Moto Wa Kuotea Mbali; Washiriki Wakiri!

Workshop ya East Africa Productive Trainers inayoendelea hivi sasa inaelezwa kuwa ni nzuri kupindukia huku wadau wakiisifia kutokana na knowledge inayotolewa, Blog hii pia imehudhuria na kulipeleka hewani tukio zima live kama ifuatavyo;
Mkufunzi akitema cheche hapa!
Hapa washiriki wakiwa makini kufatilia workshop!

Mh Chakushimire akifatilia workshop!

Hapa washiriki wakiendelea kupata knowledge

Sing To God: Joint Mass With Calvary Singers

Calvary Singers wakifanya vitu vyao jana LT1
Wadau wakimsifu Mungu
Na hapa pia "wanamsifu Mungu"



BREAKING NEWZ! MWANAFUNZI WA LAW APATA TATIZO LA AKILI! KISA RIPOTI YAKE YA DEGREE KUGOMEWA


Jengo la Faculty of law linavyoonekana kwa nje(picha ya maktaba)

Na Mwandishi Wetu Morogoro Mjini,
Habari zilizotufikia hivi punde zinabainisha kuwa mwanafunzi wa Laws wa CHUO KIKUU MZUMBE jina tunalihifadhi amepata matatizo ya akili ambayo yanadaiwa kusababishwa na msongo wa mawazo .
Habari zaidi zinaeleza kuwa jamaa huyo amehitimu Mzumbe Mbeya Branch degree ya sheria mwezi wa 7 mwaka huu lakini tangu amalize hajapata ripoti yake. Jamaa huyo anadaiwa kuhamia hapa Mzumbe ambapo alikuwa akikaa kikenge kimojawapo nyuma ya Library , Blog hii imefanikiwa kuona mlango uliovunjwa na jamaa huyo kutokana na kupatwa na tatizo la akili, mpaka tunakwenda mtamboni leo hii jamaa huyo yupo hospitali ya Rufaa Morogoro Mjini.
BLOG HII INATOA POLE KWA MWANAMZUMBE HUYO NA KUMTAKIA AFYA NJEMA!

TANZIA; BURIANI NDUGU YETU KELVIN BENDA(LLB1)


Pichani ni Marehemu Kelvin Benda,MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI....AMEN!

Friday, September 9, 2011

Mrembo Alipolizwa na Wauza Computer wa Karia Koo

Habari za kina zinadai kuna mrembo mmoja wa mwaka wa kwanza amelizwa na wauza compuer wa karia koo jijini Dar mtaa wa Tandamti ambao walitua Morogoro mjini kwa kazi zao za kuuza computer ndipo bibiye huyo "akajilengesha" kama wasemavyo watoto wa mjini.
Taarifa za kiuchunguzi zinamtaja jamaa huyo kwa jina la Eddo ambaye anadaiwa kumtelekeza binti huyo kwenye Taxi huku ikiwa na deni la shilingi elfu ishirini.