Friday, November 18, 2011

Prof Kamuzora; Si Kweli Kwamba tunalea watu wasio na maadili


Prof Faustine Kamuzora akiwa jijini New York nchini Marekani katika jengo la World Trade Centre
Siku ya tarehe 16 mwezi huu ambayo ilikuwa ni siku maalumu ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere katika chuo kikuu Mzumbe , sambamba na sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Blog hii ilimtafuta professor Kamuzora na kufanya naye mohojiano katika hotel ya Lumumba, soma zaidi...........

MUSO Link; Hongera prof Kamuzora na wanamzumbe wote kwa kuadhimisha siku hii, je wewe unaizungumzia vipi siku hii?

Prof Kamuzora; Asante , kwanza napenda nikumbushe kuwa kwa chuo kikuu Mzumbe siku hii ya Mwl Nyerere huadhimishwa kila mwaka sio mwaka huu tu, lakini pia naweza  kusema kuwa imekuwa ni siku nzuri watu wamepata muda wa kujadili kuibua mawazo na kuchangia maswala mbalimbali ikizingatiwa kuwa Mada ya leo ilihusu mtazamo wa Mwl Nyerere katika elimu ya juu.

MUSO Link; Kumekuwa na mtazamo kuwa siku hizi wasomi wamekuwa hawana maadili tofauti na enzi za Mwl Nyerere, je wewe unalizungumziaje hili?

Prof Kamuzora; Ndugu mwandishi si kweli kwamba tunafundisha au kulea watu wasio na maadili, ukweli ni kuwa hat leo hii kuna watu ambao ni waaminifu "clean" tena wana maadili halikadhalika kuna watu ambao hawana maadili, hivyo si kweli  kabisa kuwa watu wote wa kizazi hiki ni waovu.

MUSO Link; Ungependa kuwaambia nini wanamzumbe na watu wengine kuhusiana na siku hii ya Nyerere?

Prof Kamuzora; Kwanza wanamzumbe wanapaswa kufahamu kuwa hii ni siku muhimu sana ya kujadili maswala mbalimbali pia watanzania kwa ujumla wanapaswa kujadili mitazamo ya baba wa Taifa, kuipima lakini pia watu wanapaswa kuzingatia zama tulizopo "era" kwa maana zama pia zimebadilika na hata mambo yanabadilika pia.

MUSO Link; Asante Professor na nakutakia kazi njema

Prof Kamuzora; Asante pia.

No comments:

Post a Comment