Monday, December 5, 2011

Office Mpya Ya MUSO na Vita Ya Madaraka Mzumbe University



Office Mpya ya Serikali ya Wanafunzi Mzumbe imedaiwa kugeuka source ya mvutano miongoni mwa Wanamzumbe wenye lengo la kuwania urais. Habari za kina ambazo Blog hii inazo ni juu ya uwepo wa mpambano mkali miongoni mwa Wanamzumbe kugombea kukaa ndani ya ofisi hiyo.

Nchimbi ala NONDOZ ya PHD Mzumbe University


Waziri wa michezo na habari, Dkr Emmanuel Nchimba (katikati) akiteta jambo na Dkr Lushakuli Saimon kushoto na Dkr Nangawe Abbi kushoto wakati wa mahafali ya 10 ya chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro ambapo Dkr Nchimbi alitunukiwa utafiti wa dhima ya mikopo midogo midogo katika kupunguza umaskini (PHD) wakati Dkr Saimon akitunukiwa utafiti katika ubora wa vituo vya magari ya abiria vya ubungo Dar es Salaam na Msamvu Morogoro huku Dkr Abbi utafiti wa ushirika wa makampuni binafsi katika masoko ya mitaji yanayojitokeza aliofanya masoko ya mitaji Tanzania ambapo jumla watafiti saba walitunukiwa utafiti wa aina mbalimbali (PHD) katika chuo hicho mkoani hapa(Juma Mtanda Blog)

Jaji Samatta Kutunuku Wahitimu 2220 Mzumbe University; Gazeti la Habari Leo


MKUU wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta jana alitarajiwa kuwatunuku wahitimu 2,220 wa shahada mbalimbali.

Miongoni mwa wahitimu hao kwenye mahafali ya 10 ya chuo hicho mjini Morogoro wamo saba wa Shahada za Uzamivu (PhD).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chuo hicho, Rainfrida Ngatunga alisema miongoni mwa wahitimu saba wa Shahada ya Uzamivu ni Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Wengine ni Gustav Kunkuta, Simon Lushakuzi, Sunday Makama kutoka Nigeria, George Makoma, Anarabbi Nangawe na Fred Rwechengula.

“Sisi kama chuo (Mzumbe) tunajivunia sana kuona namna uwiano wa jinsia kwa wahitimu unavyoshabihiana kwani kati ya wahitimu wote 1,282 wanaume na 938 wanawake,” alisema Ngatunga na kuongeza kuwa mahafali hayo yalitanguliwa na warsha chuoni hapo juzi.

Miongoni mwa mambo yaliyotarajiwa kufanywa juzi kwenye warsha ni kutambua michango mbalimbali ya wanazuoni waliofanya vizuri kwenye masomo na utafiti.

“Chuo chetu kitachukua fursa hiyo pia kutambua mchango wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa
(NHIF) katika ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike kwenye Kampasi Kuu Morogoro,” aliongeza.

Ngatunga alisema chuo pia kinatambua mchango mkubwa na uungaji mkono wa Benki ya CRDB katika mchakato mzima wa kuandaa kongamano la wadau wa elimu la chuo hicho lililofanyika Mei mwaka huu.

Akifafanua zaidi kuhusu mahafali hayo, Ngatunga alisema miongoni mwa wahitimu hao 1,365
watatunukiwa Kampasi Kuu Morogoro, wakati 47 watatunukia Shahada za Uzamili kwenye Shule ya Biashara ya Mzumbe iliyopo Dar es Salaam Desemba 16, na 383 watatunukiwa shahada zao kwenye Kampasi ya Mzumbe Mbeya Desemba 10, mwaka huu.

MHAFALI YA 10, CHUO KIKUU MZUMBE

 

Mhitimu wa kozi ya Public Administration in Health Service Management, Enighenja Amiri akipata chakula mara baada ya kutunikiwa cheti chake.
..
Mmoja wa wahitimu akivalishwa taji na mmoja kati ya ndugu zake.
CHUO Kikuu cha Mzumbe, Morogoro jana kiliadhimisha mahafali ya 10 na wahitimu wa kozi tofauti waliweza kutunikiwa vyeti vyao.
 
Sherehe zikiendelea katika garden za chuo hicho.
Picha kwa hisani ya Global Publishers

PICHA ZOTE NA ERICK EVARIST/ GPL