Wednesday, August 31, 2011
Mzumbe Auditors' Party Umewaona Hao?
Kama Kawaida ya Blog hii siku ya jana Kamera ziliwanasa wakaguzi wa mahesabu na fedha a.k.a Auditors(PSAFI)
wakiwa kiwanja fulani walipoamua kujumuika pamoja kusherehekea Idd El fitri , sasa tufate uone tukio kamili hapa chini.........................!
wakiwa kiwanja fulani walipoamua kujumuika pamoja kusherehekea Idd El fitri , sasa tufate uone tukio kamili hapa chini.........................!
Hapa wamesahau stargard wanafurahia Idd teh teh teh!
Duuuu! cheki mambo hayo wanacheka tuuu!
Tupo pamojaaaaaa, cheki wanavyofurahi
Mwenyekiti wa PSAFI Mr Danny akitema cheche zake hapa !
Ikumbukwe kuwa wasomi hawa wa PSAFI wamejiwekea historia ya namna yake ya umoja na mshikamano haijawahi tokea tukio la namna hii, ni la kwanza hili, je Faculty nyingine mpo hapo?
Jamaa Alipovamia Idd Pasipo Kualikwa, Akodi Baiskeli na Kanzu, Ilibaki Kidogo Aumbuke, Blog hii Ikamnasa!
Katika kuonyesha kuwa za mwizi ni arobaini, jamaa mmoja ambaye anakawaida ya kuibuka kwenye sherehe pasipo kualikwa ameumbuka vibaya jana baada ya kuingia kwenye "domo la mamba"
Blo hii ilimfatilia jamaa huyo hatua kwa hatua tangu akipanda Hiace mpaka Morogoro mjini ambapo aliingia kwenye nyumba fulani maeneo ya Kihonda kisha akatoka akiwa amevaa kanzu na ghafla akaingia kwenye uchochoro fulani na kukodi baiskeli kisha safari ya "kuzamia "ikaanza.
Alipofika kwenye sherehe hiyo ambayo hakualikwa jamaaa kapaki baiskeli yake na kukaa mkekani ghafla mgawa chakula na vinywaji alipomfikia akataka kuponi, ghafla jamaa akasema kaisahau basi akahojiwa "twambie hata rangi ya kuponi" jamaa akashindwa akapaniki akataka kupigana, muda wote huo mwandishi wetu alikuwa anamfatilia ndipo jamaa kwa hasira akapanda baiskeli yake na kutokomea.
Monday, August 29, 2011
Kuelekea Idd Elfitri; TAMSA Mzumbe Watoa Tamko.....Soma Kwa Undani
Nova Kambota akiwa na Bw Rajab Semgonja Mkuu wa Habari na Mawasiliano TAMSA
Tukiwa tunaelekea sikukuu ya Idd Elfitri baada ya safari ndefu ya siku 30 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Blog hii imefanya mahojiano na Tanzania Muslim Students Association(TAMSA) chuo kikuu Mzumbe ambapo Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa TAMSA Chuo Kikuu Mzumbe Bw Rajab Semgonja alijibu maswali kadhaa kama ifuatavyo......;
MUSO Link; Baada ya safari ndefu ya siku 30 za kufunga na sasa tukiwa tunahesabu masaa kadhaa kabla ya kusheherekea Idd Elfitri, je una lipi la kusema?
Semgonja; Kwanza shukranzi ziende kwa Mwenyezi Mungu kwa kutuweka salama mpaka hatimaye tumefikia siku hii ambayo tunakaribia kusheherekea siku kuu ya Idd, pia nikiri wazi kuwa muda wote wa Ramadhani umekuwa ni kipindi kizuri kwetu waislamu kujitafakari, kuomba toba, kubadili mwenendo wetu na kumrudia Mwenyezi Mungu mweza wa yote, kwa kifupi ni kipindi ambacho kimetujenga na kutuimarisha kiimani.
MUSO Link; Ikizingatiwa kuwa Mzumbe ni sehemu ya wasomi na zaidi ni vijana pia kuna maswala kama ulevi , uasherati na mengine mengi, je unadhani mwezi wa Ramadhani ulisaidia kupambana na mambo haya kwenye jamii ya Mzumbe?
Semgonja; Ni kweli kabisa ndugu mwandishi kuwa mambo maovu kama hayo yapo, kwa upande mmoja mwezi mtukufu wa Ramadhani umetujenga sana lakini umesaidia baadhi ya watu kubadili mwenendo wao hata hivyo bado hatujafanikiwa kwa asilimia mia moja hivyo mapambano yanaendelea, tutaendelea kuwahimiza wanamzumbe waachane na uovu na kuomba toba kwa Mwenyezi Mungu.
MUSO Link; Kesho ni siku kuu ya Idd , je mmejiandaeje kusherehekea siku hiyo?
Semgonja; Kesho tutakuwa na Baraza la Idd ambapo waislamu tutakusanyika pamoja, kuswali, kupata mawaidha ya walimu,tutasheherekea pamoja na ndugu zetu kutoka Mzumbe secondary na baadhi ya wafanyakazi, sambamba na hayo tutakula pamoja na kupata wasaa mzuri wa kusikiliza nasaha kutoka kwa Maimam na walimu wa Dini yetu, hivyo tunamshukuru Mungu kuwa maandilizi ya siku kuu ya Idd yanaendelea vizuri sana.
MUSO Link; Mwishowe wewe kama kiongozi wa dini na msomi wa chuo kikuu, je nini wito wako kwa waislamu wa Mzumbe na wanamzumbe kwa ujumla?
Semgonja; Kwanza natoa wito kwa waislamu wote kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha siku hii ya Idd lakini pia natoa wito kwa kuwataka Wanamzumbe wote kila mmoja kwa nafasi yake kujitafakari, kutubu , kuwa na mwenendo mwema unaompendeza Mwenyezi Mungu.
MUSO Link; Asante kwa ushirikiano na Idd Mubarak
Semgonja; Asante ndugu mwandishi nasi kama TAMSA tunakukaribisha kwenye Baraza la Idd
Vita Ya Kumrithi Uswege Sasa Yapamba Moto, Kampeni Zaanza Kimyakimya

Utafiti wa kina ulioendeshwa na jopo la wanahabari wa Blog hii umebainisha kuwepo kwa kampeni za chini kwa chini za baadhi ya "watu" kuwania urais.
Haijafahamika mara moja iwapo watu hao wanafahamu kuwa wanafanya makosa kuanza kampeni kabla ya muda? taarifa zaidi zinaeleza kuna mikakati mitano inayotumika kufanikisha mbinu hizo;
Kwanza ni "kujichanganya na watu" mbinu hii inafanywa kwa baadhi ya watu wenye nia ya kuwania kujisogeza karibu na watu hususani sehemu ya kula, mbinu ya pili kuvaa vizuri "kulipuka" watu hao wanadaiwa kushona nguo nzuri kiasi kwamba wanataka kujenga picha kuwa wanafaa kukabidhiwa mikoba ya Uswege, mbinu ya tatu ni socialization hawa wanatumia vitu kama mechi za kirafiki kueneza propaganda zao, nne ni kuunda mitandao ya kuratibu kampeni na tano kutumia silaha ya ufaculty.
Uchunguzi zaidi unawataja wahusika wa mbinu hizi kwa faculty zao(majina tunayahifadhi lakini baadae tutayaanika) , wahusika hao ni pamoja na yule wa social science ambaye huongea kwa upole sana na ni smart kwa mavazi kupindukia, wa pili ni yule wa Laws ambaye ni mcheshi na mwongeaji sana , wa tatu ni yule wa BPA/SOPAM ambaye anapenda kushiriki kwenye midahalo ya hapa na pale na wa nne ni yule wa Commerce ambaye anajenga nertwork yake kimyakimya kwa kushirikisha baadhi ya watu maarufu hapa chuoni.
Blog hii inatoa wito kwa wahusika kuacha vitendo hivyo kwani siyo muda muafaka hivyo ni kinyume cha sheria.
Faculty Of Science&Technology Waja na Mworabaini Wa Matatizo Yao!
Viongozi wa Faculty of Science and Technology
Members wote wa Faculty of Science and Technology wamefanya kikao kinacholenga kuibua changamoto zinazoikabili faculty hiyo na kuja na suluhisho.
Hayo yalisemwa katika kikao kilichofanyika LT2 ambacho kimekuja na maazimio kadhaa yanayolenga kuifanya faculty hiyo kuwa kitovu cha wanasayansi chuo kikuu Mzumbe na Taifa kwa ujumla.
Nova Kambota; Imetosha Naomba Nijibu Hoja Sasa!
Nova Kambota
KWA KUZINGATIA KUWA MZUMBE NI JAMII YA WASOMI NA WANATAALUMA HAITEGEMEWI KUFANYA MAMBO KWA MAZOEA BALI HOJA NA MANTIKI HALIKADHALIKA UNAPOTOKEA UVUMI WOWOTE NI LAZIMA UTOLEWE MAELEZO.
KUFUATIA KUANZISHWA KWA BLOG HII YA KUNA MALALAMIKO KADHAA YAMETOLEWA AMBAYO KAMA WAZIRI WA HABARI WA MUSO NALAZIMIKA KUYATOLEA MAELEZO KAMA IFUATAVYO;
1.KWANZA KABISA BLOG HII NI MALI YA WANAMZUMBE WOTE KWA MAANA NI YA MUSO HIVYO NI MALI YA WANAFUNZI WOTE.
2.NATOA WITO KWA WANAMZUMBE KUWAPUUZA WATU WACHACHE WALIOANZA KUHOJI KWANINI IITWE musolink22 HUKU BAADHI WAKIKOLEZA UZUSHI WAO KUWA ETI MIMI NOVA NIMETIMIZA MIAKA 22 SIKU CHACHE ZILIZOPITA HIVYO KWANINI NIWEKE PERSONAL INTEREST KWENYE MUSO? NAOMBA NIELEZE 22 IMETOKA WAPI? 22 NI JUMLA YA HERUFI ZINAZOUNDA NENO "MZUMBE UNIVERSITY ELITES" UKIHESABU IDADI YA HERUFI UTAPATA 22 HIVYO HAINA UHUSIANO NA UMRI WANGU.
3. KILA MMOJA ANARUHUSIWA KUTOA MAONI AU KUHOJI CHOCHOTE NA HATA KUTUMA PICHA NA HABARI KWA NJIA YA EMAIL NASI TUTAICHAPA BILA UPENDELEO.
MWISHOWE SIHITAJI MALUMBANO KATIKA HILI BALI NATOA WITO WA KILA MMOJA WETU KUTOA MAONI YAKE TUFANYEJE ILI KUZIDI KUIBORESHA BLOG YETU HII?
ASANTENI IMETOLEWA TAREHE 30/08/2011
Nova Kambota(Waziri wa Habari-MUSO)
Sakata la Workshop ya MUEDA larindima tena ngoma bado mbichi kabisa!
Baadhi ya wanafaculty wa science and technology
senetor wa science and technology Mh Abed Ngunike
Katika hali isiyo ya kawaida malalamiko kuhusu workshop iliyofanywa na MUEDA yameibuka tena leo. Hali hiyo imejitokeza wakati wa kikao cha wanafaculty wa Science and Technology usiku wa saa nne kwenye ukumbi wa LT2.Blog hii ilifanikiwa kunasa baadhi ya malalamiko ya wachangiaji ambao walionyesha kukerwa na workshop hiyo waliyodai ipo chini ya kiwango.
EDWIN SAMSON ;DEMOKRASIA YA UKWELI HURUHUSU UHURU WA MAWAZO
Binadamu wengi huzungumzia uhuru wa mawazo lakini hawajui kuwa hakuna uhuru kamwe hapa duniani,Tulipokuwa katika harakati zetu za kugombea Urais kuna watu walijifanya eti wao ndiyo wamezaliwa kuongoza wanafunzi wenzao wa hapo chuoni,kuna kundi dogo la watu, nawaita kama watu wakupata ambao hawajui mbele wala nyuma eti wakadai Edwin ni msaliti ni mtoto wa kihuni hawezi kutuongoza sisi wazeeee wa busara.......................Kuna watu wanadhani uongozi ni sehemu ya kujichotea asali na kusahau dhamana halisi walizonazo wanazotakiwa kuwajibika kwa wananchi.HUU NI UPUUZI ETI WATU WANATIMUANA TIMUANA KISA KAPOSHO.........tulihaidiwa bomba kutoa maziwa,viwanja kuwa kama oldtraford,kila mwanafunzi kuwa na laptop .... sisi wasaliti tulikuwa tunaangalia watu wakikushabikia kumbe ni ndoto za alinacha...nawaambieni kama kuna ufisadi wowote sasa hivi nitawapeleka MAHAKAMANI, yule mshenzi MSTAAFU tulimuonea huruma ...........JAZENI MATUMBO LAKINI KUMBUKA JELA YAJA
Chuo Chetu Kinajitosheleza; Mdau Atema Cheche!
futa havard of africa acha mzumbe yenyewe kama motto tafuta nyingine
jamani tuondoleeni hilo nine havard of africa katika jina la chuo chetu mzumbe tuliosoma hapo hatuwahi kuwa na mawazo ya kufananisha chuo chetu na kikingine kwani kinajitosheleza chenyewe na mambo yake,na kinatupa mkate na heshima kote ulimwenguni,sasa nyie vizazi vyipya mmekuja na yenu,msiongerze neno kwa mzumbe.kwanza neno havard mmekosea ni Harvard ,wakija jua mnatumia jina lao watakuja juu,hebu nenda kwa waalimu wa sheria hapo chuoni uliza nenda hata kwa mama opio ni mwanasheria mzuri tu.
Onesmo Mpinzile Atetea Uamuzi Wa Mh Uswege Kumtimua Jacob.......Soma uchambuzi wake wa kisheria
Maamuzi ya Mh Uswege Kisheria
Katika taratibu za kisheria kwa maana ya Both administrative and Constitutional law, Alichokifanya Mh Uswege kinakubalika nisijue kibinadamu! Principle za Ministerial kwa maana ya (Collective na Individual) responsibility Waziri au member yeyote wa cabinet haruhusiwi kupinga jambo au hoja yoyote ya serikali bungeni, anatakiwa kufanya hivyo wakati akiwa kwenye vikao vya Cabinet (Baraza la mawaziri), anatakiwa kuonyesha hali hiyo kwa presiding cabinet chairman amabyo kwa kawaida anaweza kuwa President, Vice president au Prime Minister as the circumstance may be.
Ikiwa jambo hilo au hoja hiyo waziri au member yeyote wa cabinet anaona imeshindikana kukubalika na anaona ina maslahi kwa umma au taifa na imekataliwa kujadiliwa na baraza hilo au imetupiliwa mbali!!...Basi mjumbe huyo wa baraza ataamua kujiudhru uwaziri au ujumbe wa baraza ili ajadili jambo hilo kama mbunge...na katika hali hiyo atakuwa huru kulipinga kwa nguvu zake zote. Kama hatajiudhuru wadhifa huo kwanza na akapinga, sheria inasema kwamba President atatakiwa kumfukuza kazi...Jambo la kumfukuza kazi ni discreationlly (au lipo ndani ya maamuzi ya rais, anaweza kufanya hivyo au asifanye hivyo). Hana obligation (ulazima ) wa kumfuta kazi, n hakuna ulazima wa yeye kufanya hivyo...
Jambo hili si jipya liliwahi kutokea hapa Tanzania na nchi nyngi za jumuiya ya madola, mfano miaka ya 1987-89 Kingunge Ngombale Mwilu wakati akiwa Regional Commissioner, 1993 Mh Augustine Lyatonga Mrema alilazimika kujiudhuru uwaziri kutokana na kutoridhika na maamuzi ya jambo kwenye baraza a mawaziri, Pia angalizo hilo lipo katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, 1977, ambayo inasema 'the Minister shall assume office at the pleasure of the President'.
Hivyo kisheria jambo hilo lipo sahihi nisijue mchango wa Jaju katika baraza la Mh Uswege .
Hivyo kisheria jambo hilo lipo sahihi nisijue mchango wa Jaju katika baraza la Mh Uswege .
Mpinzile S. Onesmo
+255714702824
+255785702824
craddleb@yahoo.com
craddletz@gmail.com
Mzumbe University, Bachelor of Laws
Mororogoro Tanzania.
Friday, August 26, 2011
BEAKING NEEEWZ! Banzi Azua Balaa ni baada ya Mrembo Mmoja Wa UDOM kutishia Kujinyonga Akimlilia Rais Huyo Mstaafu Wa MUSO!
Habari kutoka chini ya kapeti zinadai kuwa Rais Mstaafu wa MUSO Bw Raphael Banzi ameponea chupuchupu kutinga panapo lupango mara baada ya mrembo mmoja anayesoma chuo kikuu cha Dodoma kutishia kujitia kitanzi akililia penzi la Bw Banzi.
Habari za kina kutoka kwa chanzo chetu ambacho kiko karibu na Banzi kinadai "kweli kaka yule dem kamlilia sana jamaa ila jamaa kabana mpaka mwisho sasa dem alitaka kujinyonga"
Habari zaidi zinaeleza kuwa Bw Banzi ambaye anahusishwa na familia ya kidini yenye Askofu mmoja aliamua kumwekea ngumu mrembo huyo ambaye naye aliona hawezi kuishi bila penzi la Banzi ndipo alipoamua kujipeleka kuzimu kabla ya muda wake kufika , zoezi ambalo hata hivyo liligonga mwamba na mrembo huyo yungali bukheri wa afya.
Mpaka tunakwenda mtamboni hatujafanikiwa kuzungumza na Banzi juu ya taarifa hizi, simu yake haikupatikana kwa zaidi ya mara tatu tulipojaribu kumtafuta.
BLOG HII INATOA POLE KWA BW BANZI KWA MASAIBU HAYO YALIYOMFIKA
Subscribe to:
Posts (Atom)