Sunday, August 21, 2011

SAKATA LA WORKSHOP YA ENTERPRENUERSHIP :MWENYEKITI MUEDA ASHIKILIA MSIMAMO WAKE, WASHIRIKI WADAI PESA ZAO, MUSO YAHUSISHWA NI VURUGU MECHI TUPU!

Kutokana na mvutano ulioibuka siku ya jana kati ya washiriki na viongozi wa MUEDA kutokana na washiriki wa workshop hiyo kulalamika vikali wakidai kutapeliwa tayari hali ya mambo imezidi kuchafuka kabisa.

Akizungumza na blog hii ya MUSO Link mwenyekiti wa MUEDA Bw Baraka Mwilapwa amekanusha vikali kuhusika na ubadhirifu wa aina yoyote, fuatilia mahojiano hayo na mwenyekiti wa MUEDA ili ufahamu undani wa sakata hilo;

MUSO link; Ndugu mwenyekiti wa MUEDA kwanini mmedanganya watu kuwa kuna wanataalamu kama prof kamuzora wangeshiriki lakini hawakuwepo?

Baraka; Hakuna ukweli wowote juu ya hilo isipokuwa ni kweli walisema wangehudhuria lakini kwa bahati mbaya ni kuwa hawakuweza kufika na walinipa taarifa.

MUSO link; Je baada ya wanataaluma hao kusema hawatahudhuria je kwanini hukutoa taarifa kwa washiriki?

Baraka; Nikiri wazi kuwa ni kweli walinipa taarifa lakini nilishindwa kuwajulisha washiriki kwasababu nilihofia kuharibu mood yao.

MUSO link; Kuna baadhi ya washiriki wanadai MUSO inahusika katika sakata hili, je wewe unaliongeleaje?

Baraka; Niseme jambo moja kuwa MUSO haihusikiki na MUEDA hivyo hakuna sababu yoyote ya kuihusisha MUSO na mambo ya MUEDA.

MUSO link; Ndugu Baraka unakubali kuwa kama mwanafunzi ukifanya mtihani unajua aidha umefeli au umafaulu, sasa washiriki wanaona huduma iliyotolewa na pesa walizolipa ni kama kaskazini na kusini, je wewe unasemaje?

Baraka; Jambo pekee naloweza kusema ni kuwa watu walinipongeza sana lakini huo uvumi unaonezwa ni upuuzi wa watu wachache tu ambao walitaka wapewe mambo fulani fulani lakini wamekosa , ni lazima wajue kuwa hii ni taasisi siyo mali ya mtu hivy mambo yanaenda kwa kanuni siyo ushabiki.

MUSO link; Mwishowe unawaambia nini wanamzumbe? na washiriki wote wa workshop?

Baraka; Nawaambia wanamzumbe kuwa kinachomatter ni knowledge siyo misosi hivyo wafurahie kupata mind liberation siyo vitu consumable kama vyakula na vinywaji.

Haya sasa mdau unasemaje kuhusu sakata hili tupe maoni yako...!



Mh Uswege Isaac; Mawaziri Wote Lazima Wahudhurie Kikao Leo!

Rais wa MUSO Mh Uswege Isaac amesisitiza kuwa ni lazima mawaziri wote wahudhurie cabinet meeting. Akizungumza na blog hii leo Mh Uswege amesisitiza kuwa kuhudhuria kikao ni lazima sio ombi.
 Tulipotaka kufahamu kwanini amekuwa kali hivyo? yeye alisisitiza tu kuwa "MAWAZIRI WOTE LAZIMA WAHUDHURIE KIKAO FULL STOP"

BREAKING NEEWZ! MWIZI ANASWA NA KAMERA ZA LIBRARY


Kama ulikuwa hujui sikia hii kutoka jengo hilo hapo juu kuna sakata la aina yake limetokea Library baada ya jamaa mmoja kunaswa na kamera za Library akikwapua simu.

Taarifa za ndani kutoka kwa chanzo chetu mmoja wa wafanyakazi wa Library zinadai kuwa jamaa huyo ni mwaka wa kwanza ambaye amenaswa live na kamera akikwapua simu hiyo.

 Akielezea sakata hilo mfanyakazi huyo wa Library amekaririwa akisema..."mimi nakwambia hivi huyu mtoto ana tatizo gani amekuja huku kusoma au kuiba? "

Habari za utafiti zinaweka bayana kuwa hata serikali ya MUSO inafahamu kuhusu jambo hilo lakini bado haijafahamika ni hatua zipi MUSO imechukua?

Mpaka tunakwenda mtamboni muda huu tuna taarifa rasmi kuwa mhusika wa uhalifu huo tayari ametiwa nguvuni, na mwandishi wetu anafatilia kwa karibu ili kubaini hatua zipi zitachukuliwa dhidi yake.

Mdau Angelo !


Mdau Angelo huyu hapa , leo tumemnasa na kamera zetu alikuwa anashangaa!

Mawaziri Wa MUSO Waanza Kujipanga Upya

Wataalamu wa mambo ya utawala wanakubaliana kuwa sometimes kwenye maisha kuna ukweli mchungu lakini lazima usemwe tu, naam! huu ndiyo ukweli wenyewe kwamba kufuatia malalamiko yasiyokwisha ya wanafunzi sasa mawaziri wa MUSO wameanza kujipanga upya kuja na mikakati kadhaa, tumejulishwa kuwa tayari Cabinet inakutana leo usiku.

Ona Picha Hii, Ina Tafsiri Gani?


Mdau look ! hii ni picha nzuri inafurahisha sana,picha moja tafsiri 1000, je hii picha ina tafsiri gani?

Saturday, August 20, 2011

BREAKING NEEEWZ! WAZIRI MKUU AAMUA KUSAMBAZA PICHA BAADA YA WATU KUHOJI


Blog hii imefanikiwa kumhoji waziri mkuu wa MUSO Mh Benson Futte ambaye ametueleza bayana kushtushwa na watu kuhoji muonekano wake huku baadhi wakitaka kufahamu anafananaje? sasa Mh huyu ameamua kusambaza picha zake ili watu wamfahamu vizuri na kuacha kuhoji swali la anafananaje? ambalo amekiri swali hilo linamkera na kumkosesha raha.

TAARIFA KWA UMMA; KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI


Taarifa kwa Viongozi wote wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe kuwa Kutakuwa na Cabinet Meeting siku ya kesho yaani jumapili tarehe 21 August 2011.

Ajenda za kikao hiko ni pamoja na ;
1. Opening Meeting
2.Speech from The President
3.Brief MUSO Budget
4.AOB
5.Closing The Meeting
TAARIFA ZAIDI ZITAENDELEA KUTOLEWA KUPITIA MBAO ZA MATANGAZO
Imetolewa na MUSO G.S

Tuesday, August 16, 2011

Kuelekea Bunge la Bajeti; Yuko Wapi Mh Futte?


kutoka kushoto ni waziri mkuu wa MUSO Mh Benson Futte
Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kuitishwa kwa Bunge la Bajeti la serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe tayari watu wameanza kuhoji alipo waziri mkuu Mh Benson Futte.
Hali hiyo inakuja kukiwa na hamu kubwa ya kuona wabunge wakichemshana kwa hoja katika week chache zijazo.

Wanamzumbe Wajikumbusha Kampeni za Uswege

Katika hali isiyo ya kawaida kumeibuka minong'ono juu ya uongozi wa rais wa sasa wa MUSO Bw Uswege Isaac huku baadhi wakihoji juu ya utendaji wake. Utafiti ulioendeshwa na blog hii umebaini kuwa hasira zote hizo za baadhi ya wanamzumbe zinakuja huku kukiwa na madai ya fedha za kujikimu kutoka kwa baadhi ya wanafunzi ambao wanadai hawajapata fedha za kujikimu mpaka leo.
Baadhi yao wamesikika wakiongea kwa huzuni kubwa huku wakikumbushia kampeni za Mh Uswege