Monday, August 29, 2011

Sakata la Workshop ya MUEDA larindima tena ngoma bado mbichi kabisa!

Baadhi ya wanafaculty wa science and technology
senetor wa science and technology Mh Abed Ngunike
Katika hali isiyo ya kawaida malalamiko kuhusu workshop iliyofanywa na MUEDA yameibuka tena leo. Hali hiyo imejitokeza wakati wa kikao cha wanafaculty wa Science and Technology usiku wa saa nne kwenye ukumbi wa LT2.
Blog hii ilifanikiwa kunasa baadhi ya malalamiko ya wachangiaji ambao walionyesha kukerwa na workshop hiyo waliyodai ipo chini ya kiwango.

EDWIN SAMSON ;DEMOKRASIA YA UKWELI HURUHUSU UHURU WA MAWAZO


Binadamu wengi huzungumzia uhuru wa mawazo lakini hawajui kuwa hakuna uhuru kamwe hapa duniani,Tulipokuwa katika harakati zetu za kugombea Urais kuna watu walijifanya eti wao ndiyo wamezaliwa kuongoza  wanafunzi wenzao wa hapo chuoni,kuna kundi dogo la watu, nawaita kama watu wakupata ambao  hawajui mbele wala nyuma eti wakadai Edwin ni msaliti ni mtoto wa kihuni hawezi kutuongoza sisi wazeeee wa busara.......................Kuna watu wanadhani uongozi ni sehemu ya kujichotea asali na kusahau dhamana halisi walizonazo wanazotakiwa kuwajibika kwa wananchi.HUU NI UPUUZI ETI WATU WANATIMUANA TIMUANA KISA KAPOSHO.........tulihaidiwa bomba kutoa maziwa,viwanja kuwa kama oldtraford,kila mwanafunzi kuwa na laptop .... sisi wasaliti tulikuwa tunaangalia watu wakikushabikia kumbe ni ndoto za alinacha...nawaambieni kama kuna ufisadi wowote sasa hivi nitawapeleka  MAHAKAMANI, yule mshenzi MSTAAFU tulimuonea huruma ...........JAZENI MATUMBO LAKINI KUMBUKA  JELA YAJA

Chuo Chetu Kinajitosheleza; Mdau Atema Cheche!


futa havard of africa acha mzumbe yenyewe kama motto tafuta nyingine

jamani tuondoleeni hilo nine havard of africa katika jina la chuo chetu mzumbe tuliosoma hapo hatuwahi kuwa na mawazo ya kufananisha chuo chetu na kikingine kwani kinajitosheleza chenyewe na mambo yake,na kinatupa mkate na heshima kote ulimwenguni,sasa nyie vizazi vyipya mmekuja na yenu,msiongerze neno kwa mzumbe.kwanza neno havard mmekosea ni Harvard ,wakija jua mnatumia jina lao watakuja juu,hebu nenda kwa waalimu wa sheria hapo chuoni uliza nenda hata kwa mama opio ni mwanasheria mzuri tu.

Onesmo Mpinzile Atetea Uamuzi Wa Mh Uswege Kumtimua Jacob.......Soma uchambuzi wake wa kisheria

Maamuzi ya Mh Uswege Kisheria

Katika taratibu za kisheria kwa maana ya Both administrative and Constitutional law, Alichokifanya Mh Uswege kinakubalika nisijue kibinadamu! Principle za Ministerial kwa maana ya (Collective na Individual) responsibility Waziri au member yeyote wa cabinet haruhusiwi kupinga jambo au hoja yoyote ya serikali bungeni, anatakiwa kufanya hivyo wakati akiwa kwenye vikao vya Cabinet (Baraza la mawaziri), anatakiwa kuonyesha hali hiyo kwa presiding cabinet chairman amabyo kwa kawaida anaweza kuwa President, Vice president au Prime Minister as the circumstance may be.
Ikiwa jambo hilo au hoja hiyo waziri au member yeyote wa cabinet anaona imeshindikana kukubalika na anaona ina maslahi kwa umma au taifa na imekataliwa kujadiliwa na baraza hilo au imetupiliwa mbali!!...Basi mjumbe huyo wa baraza ataamua kujiudhru uwaziri au ujumbe wa baraza ili ajadili jambo hilo kama mbunge...na katika hali hiyo atakuwa huru kulipinga kwa nguvu zake zote. Kama hatajiudhuru wadhifa huo kwanza na akapinga, sheria inasema kwamba President atatakiwa kumfukuza kazi...Jambo la kumfukuza kazi ni discreationlly (au lipo ndani ya maamuzi ya rais, anaweza kufanya hivyo au asifanye hivyo). Hana obligation (ulazima ) wa kumfuta kazi, n hakuna ulazima wa yeye kufanya hivyo...

Jambo hili si jipya liliwahi kutokea hapa Tanzania na nchi nyngi za jumuiya ya madola, mfano miaka ya 1987-89 Kingunge Ngombale Mwilu wakati akiwa Regional Commissioner, 1993 Mh Augustine Lyatonga Mrema alilazimika kujiudhuru uwaziri kutokana na kutoridhika na maamuzi ya jambo kwenye baraza a mawaziri, Pia angalizo hilo lipo katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, 1977, ambayo inasema 'the Minister shall assume office at the pleasure of the President'.
Hivyo kisheria jambo hilo lipo sahihi nisijue mchango wa Jaju katika baraza la Mh Uswege .

Mpinzile  S. Onesmo
+255714702824
+255785702824
craddleb@yahoo.com
craddletz@gmail.com
Mzumbe University, Bachelor of Laws
Mororogoro Tanzania.

Friday, August 26, 2011

BEAKING NEEEWZ! Banzi Azua Balaa ni baada ya Mrembo Mmoja Wa UDOM kutishia Kujinyonga Akimlilia Rais Huyo Mstaafu Wa MUSO!

Na Reporter wetu Morogoro Mjini,
Habari kutoka chini ya kapeti zinadai kuwa Rais Mstaafu wa MUSO Bw Raphael Banzi ameponea chupuchupu kutinga panapo lupango mara baada ya mrembo mmoja anayesoma chuo kikuu cha Dodoma kutishia kujitia kitanzi akililia penzi la Bw Banzi.
Habari za kina kutoka kwa chanzo chetu ambacho kiko karibu na Banzi kinadai "kweli kaka yule dem kamlilia sana jamaa ila jamaa kabana mpaka mwisho sasa dem alitaka kujinyonga"
Habari zaidi zinaeleza kuwa Bw Banzi ambaye anahusishwa na familia ya kidini yenye Askofu mmoja aliamua kumwekea ngumu mrembo huyo ambaye naye aliona hawezi kuishi bila penzi la Banzi ndipo alipoamua kujipeleka kuzimu kabla ya muda wake kufika , zoezi ambalo hata hivyo liligonga mwamba na mrembo huyo yungali bukheri wa afya.
Mpaka tunakwenda mtamboni hatujafanikiwa kuzungumza na Banzi juu ya taarifa hizi, simu yake haikupatikana kwa zaidi ya mara tatu tulipojaribu kumtafuta.
BLOG HII INATOA POLE KWA BW BANZI KWA MASAIBU HAYO YALIYOMFIKA

Jaju na Uswege tatizo ni Uongozi tu au Kuna Lingine Zaidi?

Pengine kuna bundi ameanza kulia ofisi ya MUSO, ndiyo ni bundi ndiyo maana tunashindwa kuelewa kuna tatizo gani kati ya Jacob Julius na Uswege Isaac ambao wamewahi kufanya kazi pamoja tena nathubutu kusema "ni marafiki wa siku nyingi hawajakutana njiani tu"
Tunashangazwa na vuta nikuvute ya sasa tena kupitia mtandao wa facebook ambapo Bw Jacob Julius anaendeleza mapambano yake aliyoyapachika jina la "WAR AGAINST UFISADI" huku licha ya kuandika kwa mafumbo wenye uzoefu wa maswala ya uandishi tunaelewa kuwa kwa mlango wa nyuma anailenga MUSO lakini kwa mlango wa mbele anamlenga Uswege, kuamini nayosema hebu soma ujumbe huu.............."Meya Mzumbe


Nashauri utaratibu wa kulipana posho zisizo na tija kwa viongozi wa Chuo uondolewe rasmi,huku ndiko tunakojifunzia uwizi na ufisadi.Imagine mtu yupo likizo kwa sasa lakini kila mwisho wa mwezi anapewa posho ya mawasiliano mana ndivyo Bunge ...lilivyobariki,sasa nauliza mtu huyu anawasiliana na nani wakati yupo likizo?HILI NDILO LILILOSABABISHA MAWAZIRI KUMTISHIA USWEGE KWAMBA WATAJIUZULU ENDAPO HATA NIWAJIBISHA,NAMI NIKAMSHAURI ASIWE NA SHAKA YOYOTE MIMI NIKO FLEXIBLE NA HURU HIVYO AAMUE KULINDA MASLAHI YA SERIKALI YAKE,NAYE AKAONA MASLAHI YA SERIKALI YAKE NI KUNIONDOA BARAZANI,NI JAMBO JEMA TENA LA KHERI ILA SASA TUTAHITAJI MJADALA WA WAZI KUJADILI HAYA MAPOSHO WANAYOLIPANA KILA MWISHO WA MWEZI MANA BADO HAIJANIINGIA AKILINI KABISA"
lakini pia soma na ujumbe huu "Meya Mzumbe CCM lazima ianze sasa kupinga uwizi na ufisadi kuanzia kwenye mizizi yaani vyuo vikuu,nikiwa mmoja wa viongozi wastaafu wa CCM Chuo kikuu Mzumbe,sipo tayari kuona chama changu kinakufa na sipo tayari kuona wanaCCM vyuoni tunajifunza kutumia vibaya mali za wanafunzi wenzetu maana kwa kufanya hivyo tunawapa ajenda wapinzani na kuhatarisha ustawi wetu na nguvu yetu kwenye taasisi nyeti kama vyuo vikuu.Jacob Julius(JaJu)"

au soma hapa "
HOJA:wanamzumbe naomba msaada wenu wa kifikra,ni nani anayeweza kukadiria mapato yatokanayo na PRINTER ya MUSO kwa siku?
Plz tafakari kwanza kabla ya kupost koment."
Huo ni ujumbe wa Bw Jacob Julius maarufu kama Jaju katika mtandao wa facebook, sasa sisi hatudhani kama kufutwa uwaziri ndiyo kiini cha haya malumbano, tunataka tuambiwe black and white, kuna nini kati ya watu hawa wawili? tatizo ni uongozi au kuna lililo nyuma ya pazia?



BREAKING NEEWZ! MH HASSAN MASSAWE HOI MAFOMU YAMDODEA MKONONI BAADHI YA MA-CR WADAI POSHO!

Kama ulidhani uongozi wa MUSO ni lele mama a.k.a cha mtoto basi muulize waziri wa afya Mh Hassan Massawe ambaye amekumbwa na kigingi cha kwanza kutoka kwa ma-cr. Habari za uhakika zinadai kuwa waliomtia mkosi Bw Massawe ni maclass representative kutoka faculty of science and technology ambao ni ICTM, POM na A.S

Habari zinadai kuwa Bw Massawe alikuja na idea yake ya kukusanya maoni kuhusu dispensary na huduma za afya ambapo aliandaa fomu na kuwakabidhi ma cr ili watu wajaze ndipo kinyume na mategemeo yake ma cr wa science na technology wametaka posho kwa madai kuwa wapo busy na kusambaza fomu ni kazi nzito, naye Massawe akajibu kwa hasira kuwa MUSO haina pesa na ma cr wamemsusia, mpaka tunaenda mtamboni usiku huu mafomu ya Bw Massawe yamerundikana pale MUSO Office.

Ni Lini Viongozi wa MUSO wataona umuhimu wa Kuhamia Kwenye Ofisi Yenye Hadhi Yao

Pichani juu ni baadhi ya viongozi wa MUSO wakiwa na viongozi wa kitaifa(mawaziri wa serikali ya Tanzania) na picha chini ni ofisi ya MUSO(ambayo haina hadhi)
Kila mwenye kuitakia mema serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe anajihoji ni lini serikali ya Mh Uswege itaona umuhimu wa kuhamia kwenye OFISI ZA MAANA?

Kutana na Gudluck William Kijana Mwenye Vipaji Lukuki

Naam! sasa hapa sijui anaigiza au anaongea huyo ndiyo Gudluck William mbunge wa MUSO mwenye vipaji lukuki, sasa hivi punde nimemdaka akichora picha nzuri sana, ipo siku nitamwomba anisaidie kuchora picha kisha tuziweke hapa mtandaoni

BREAKING NEEWZ Prof Kamuzora Atundikwa Kwenye Group Ya Wakata KIU

Kama unadhani natania basi hayaa...! kwa maana taarifa za utafiti za Blog hii zinaonyesha kuwa group ya facebook ya wakata kiu Mzumbe inatumie picha ya profile hiyo hapo juu ambayo kimsingi ni ya prof Kamuzora, sasa haijajulikana iwapo kamuzora mwenyewe anafahamu hilo au?

Website ya Chuo Kikuu Mzumbe Inahitaji Matengenezo Upya

Website ya chuo kikuu Mzumbe www.mzumbe.ac.tz inahitaji matengenezo makubwa ya haraka, MUSO Link inaripoti bila wasi...

Uchunguzi uliofanywa na blog hii umebaini kuwa website ya chuo kikuu mzumbe haina updates za mara kwa mara, wakizungumza na blog hii baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe wamedai kufadhaishwa sana na udhaifu wa website hiyo huku wakisema wazi kuwa inabidi mabadiliko ya haraka yafanyike ili matokeo yawekwe humo pamoja na taarifa mbalimbali za kila siku.

Kuna Utata Hapa Mawaziri Wamelala Au Wamefumba Macho Tu?

Picha moja maelezo elfu moja, ona mawaziri hawa wa MUSO sijui wamefumba macho au wamelala tu?