Friday, August 26, 2011

Spika wa MUSO Mh Asifiwe Afunguka Rasmi na Kukiri Udhaifu Wa Bunge Analoliongoza, Adai halina Kanuni wa Ulinzi Kila dakika ni Mwongozo wa spika!

Spika wa bunge la wanafunzi chuo kikuu Mzumbe Mh Asifiwe Alinanuswe kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake amejitokeza hadharani na kukiri kuwa Bunge la MUSO ni "zigo zito" kutokana na kuongozwa bila kanuni wala ulinzi hali inamfanya kusimamia kila kitu muda wote.
Alikuwa anazungumza na blog hii mapema leo asubuhi ambapo alitolea mfano tabia ya kelele za wabunge "mwongozo wa spika.....mwongozo wa spika" kelele ambazo amedai ni matokeo ya kukosekana kwa kanuni za bunge.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi mkubwa kwenye srikali ya MUSO kukiri hadharani udhaifu wa bunge la MUSO.

Thursday, August 25, 2011

Mh Jacob Julius ; Afutwa uwaziri rasmi, Mh Uswege asema ana imani na baraza lake, hatishwi wala hatishiki!, Jacob Jaju ajibu mapigo kupitia Facebook

Baada ya aliyekuwa waziri wa protocal / Itifaki Mh Jacob Julius kufutwa rasmi uwaziri kwa kosa la utovu wa nidhamu huku akihusishwa na kuipinga serikali anayoitumikia , hali ya mambo sasa imekuwa vuta nikuvute huku Mh rais Uswege Isaac yeye akisema kuwa ana imani kubwa na mawaziri wake hivyo hatishwi wala hatishiki kamwe.

Huku Mh Uswege akibainisha msimamo wake, naye Bw Jacob Julius amejibu mapigo kupitia mtandao wa facebook huku akitumia jina la Meya Mzumbe katika page ya Mzumbe University, ujumbe huo unasomeka hivi..............
Tanzania inahitaji wapinga rushwa na wapinga matumizi mabaya ya fedha za umma,hao watu hawatashushwa kutoka hewani ni lazima watokee kwenye vyuo vikuu.Sifa ya kupinga matumizi mabaya ya fedha za umma siyo lazima uwe wa chama cha upinzani bali lazima uwe mzalendo.TAZAMENI BUNGE LA TANZANIA LA SASA...
 

Hotuba ya Waziri wa Fedha; Matumaini Kibao!

Waziri wa fedha wa MUSO Mh Alex Getang'ita akisoma hotuba yake Bungeni

MZUMBE UNIVERSITY STUDENTS ORGANIZATION (MUSO)

MINISTRY OF FINANCE, PLANNING AND INVESTMENT.



HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHESHIMIWA GETANG’ITA ALEXANDER NYANCHINI (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2011/2012.

TAREHE 22-08-2011

UTANGULIZI:                               

1. Mheshimiwa spika,naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu likubali kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya serikali ya mwaka wa fedha 2011/2012.Pamoja na hotuba hii yapo majedwali yanayoonyesha makisio ya mapato na matumizi.

2. Mheshimiwa spika, awali ya yote napenda kumpongeza Rais wa serikali ya wanachuo kikuu Mzumbe Mh.Uswege Isaac Mwakabonga, kwa kuchaguliwa kuongoza MUSO akiwa rais wa awamu ya kumi. Aidha ninamshukuru sana mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyonayo kwangu kwa kunichagua kuongoza wizara kubwa na nyeti, ninamuahidi kuwa sitamuangusha. Pia ninampongeza Mh.Happy Joseph kwa kuchaguliwa kuwa makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe. Vilevile naendelea kutoa pongezi kwa  Mh. Benson Fute (Mb),kwa kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe. Natoa ahadi ya kushirikiana naye kwa karibu kama mtendaji mkuu wa serikali katika kuhakikiksha tunatenda yale yote Rais aliyotuamini kwayo.

3.Mheshimiwa spika, napenda kukupongeza wewe binafsi kwa kuchaguliwa kuwa spika, na hivyo kuwa mwanachuo wa kwanza wa shahada ya pili (masters) kuongoza bunge hili tangu chuo hiki kilipopata hadhi ya kuwa chuo kikuu.Kuchaguliwa kwako kunatokana na imani kubwa waliyonayo waheshimiwa wabunge kwa kuzingatia busara zako,uwezo na uzoefu wako.Napenda pia kumpongeza Mh. Suzan Kuzilwa kwa kuchaguliwa kuwa naibu spika,nawapongeza pia mawaziri wenzangu wote pamoja na Naibu mawaziri wote, kwa kuteuliwa kwao na Mh.Rais kushika nyadhifa hizo. Aidha, napenda niwapongeze wabunge wote kwa kuchaguliwa na kuteuliwa kuwawakilisha wanachuo wenzetu katika bunge hili, chombo ambacho maamuzi makuu yanayohusu ustawi wa wanachuo kikuu Mzumbe.

4. Mheshimiwa Spika,naomba kwa namna ya pekee niwashukuru Mh.Mabula R. Mabula,Naibu waziri wizara ya fedha na katibu mkuu wa wizara ya fedha Mh. Nanzia Rajab kwa kazi ngumu waliyofanya katika kuandaa bajeti hii.

5. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa kazi wanazofanya wawakilishi wa madarasa (CR’S), serikali hii imeonelea ni vyema kuwatia motisha angalau kwa posho kidogo hata za mawasiliano kama kifuta jasho cha kazi nzito wanazozifanya. Hii itakuwa ni serikali ya kwanza tangu chuo hiki kianzishwe, kutoa posho kwa wawakilishi wa madarasa (CR’S). Kulingana na ufinyu wa bajeti yetu, kiasi cha fedha walichotengewa si kikubwa sana lakini ni mwanzo mzuri ambao ninaamini kama serikali zijazo zikiufuata na kuuboresha utaleta tija katika ufanisi wa kazi za hawa waheshimiwa.

6.Mheshimiwa Spika, kwa kipindi kirefu chuo kikuu Mzumbe, kimekuwa kikijiweka kando na masuala ya kitaifa ambayo tumekuwa tukiona vyuo vingine vikijihusisha siku hadi siku, serikali hii imejikita sana katika kuwawezesha wana wanachuo kikuu Mzumbe kushiriki katika masuala ya kitaifa na serikali imejipanga kuhakikisha inafanikisha adhima hii ikishirikiana na menejimenti ya chuo ya chuo kikuu Mzumbe.

7. Mheshimiwa Spika, katika bajeti hii serikali imeweka kipaumbele kuiboresha tovuti, ya MUSO ambayo hadi sasa  iko katika hali nzuri, napenda kumpongeza mheshimiwa Waziri husika kwa kazi nzuri anayoifanya.

8. Mheshimiwa Spika,ninayo furaha pia kusimama hapa mbele ili kutoa matazamio ya serikali kwa upande wa mapato na matumizi kwa kipindi cha mwaka mmoja wa madaraka. Bajeti ninayokwenda kuisoma punde imeangalia nyanja zote muhimu kwa maslahi ya wanafunzi wote wa chuo kikuu Mzumbe na hivyo napenda kutanguliza ombi langu kwa waheshimiwa wabunge kuwa makini sana kuchangia kwa mawazo ya kujenga na hatimaye kuipitisha ili wanafunzi wenzetu ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kutoona matunda ya pesa zao, kupitia bajeti hii, sasa wakapate kuona matunda hayo.

Naomba nichukue fursa hii sasa niweze kusoma makadirio ya mapato na matumizi ya serikali ya chuo kikuu Mzumbe kwa mwaka wa fedha 2011/2012 kwa kuzingatia mchanganuo wa kila wizara.







MHESHIMIWA SPIKA NAOMBA KUTOA HOJA.

TANZIA MZUMBE UNIVERSITY PROF NJUNWA AAGA DUNIA

BLOG HII NA WANAFUNZI WOTE WA CHUO KIKUU MZUMBE WANAYO HUZUNI KUBWA KUPOKEA TAARIFA ZA MAJONZI KUFUATIA KUFARIKI DUNIA KWA MSOMI NA MWANATAALUMA PROFESSOR MUJWAHUZI NJUNWA ALIYEAGA DUNIA KWA UGONJWA WA KISUKARI SIKU YA JANA. PROF NJUNWA ATAKUMBUKWA KWA MCHANGO WAKE MKUBWA KATIKA SCHOOL OF PUBLIC ADMINISTRATION CHUO KIKUU MZUMBE...............BWANA ALITOA, NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE,NA MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU...AMEN!

Mh Ridhia ; Another Iron Lady, Aweka Rekodi ya kuwa Mbunge wa Kike wa Mwisho kutoka Bungeni, Mwashibanda Aongoza zoezi la kumchangia

Umewahi kumwona huyo dada hapo pichani? mwangalie vizuri tuuuuu, huyo ni Iron Lady Ridhia, ambaye ameweka rekodi ya kuwa mbunge mwanamke kutoka bungeni mnamo saa nane usiku, ndipo Mh Mwashibanda akaongoza harembee ya kumpongeza kwa kumchangia pesa za pongezi, naam! huyo ndiyo Iron Lady Ridhia

Wabunge walimchachafya spika akashindwa kunywa soda yake





Katika kile kinachoonekana kuzidiwa na rabrasha za wabunge inaelezwa kuwa spika alishindwa kunywa soda yake kama anavyoonekana pichani, mpaka BUNGE linaisha Mh huyo hakuweza kuinywa soda hiyo, na hata tulipombana atueleze sababu za kushindwa kunywa soda hiyo yeye aliishia kucheka hatua inayozidi kushawishi kuwa kuongoza bunge si lelemama

Engineer mkuu wa Blog ya MUSO , viva Nova Kambota....!!

Huyu ni Nova Kambota waziri wa mawasilianona Engineer mkuu wa MUSO link akitake note Bungeni, anachukua hoja hapa! heko Nova viva Nova

Mh Temba ; Sauti Ya Upole Hoja Nzito

Kama ulikuwa hufahamu Mh Uswege hajui kuteua mawaziri basi umekosea, nasema hesabu maumivu, je unamfahamu Mh Temba mwone pichani, anasifika kwa kuzungumza kwa sauti ya upole lakini yenye hoja nzito kama sio ujumbe mkubwa.

Unawajua Maveteran wa Siasa za Mzumbe?

Mh Benson Futte waziri mkuu naye yupo kwenye list ya maveteran

Mkongwe Frank Mushi naye ni veteran pia
Vijana wa kazi hawa wabunge hai bungeni wana changamoto za kuitikisa serikali
Wengine hao ni maveteran pia ni wakongwe katika anga za Mzumbe University

Mwashibanda Eloish Mwashibanda na maamuzi magumu

Mh Mwashibanda ameonyesha msimamo wake mara kadhaa bungeni mara baada ya kunukuliwa akianika msimamo wake hadharani, mwone hapa kwenye picha alikuwa akichangia.

Spika wa bunge anawaapisha wabunge wapya mara baada ya Mh Mwashibanda kuchangia juu ya uhalali wa baadhi ya wabunge
Hapa Mwashibanda akanena "Jacob is the great person at Mzumbe lakini kama asipofukuzwa mpaka kesho saa nne mimi pia najiuzulu"
Spika akiendelea na shughuli za bungeni mara baada ya Mwashibanda kuchangia
Baadhi ya makatibu wakifurahia hoja za Mwashibanda ndani ya bunge

Wasemavyo Watani kuhusu Mh Uswge na Mawaziri Wake

Mhh! Mh Kamana unawaza nini? au swaumu kali mkuu..........


Ninyi mawziri wangu mimi nawasikiliza saaana jamani mnanifurahisha sana aisee ila ................!
Mh Uswege nasema hiviiiii...embu nisikilize kwanza............!



Tupo makini tunasikiliza tunafatilia ila aaah! hii stagered itatuua aisee...!

Hivi nyinyi mnavyoniona mkimya mnadhani sijui kubishana eenh! sasa ngojeni niwaoneshe...!

Cabinet Meeting; Ni Hoja Kwenda Mbele

Hii ni picha iliyonaswa na kamera zetu wakati kikao cha baraza la mawaziri kikiendelea, inaelezwa kuwa hapa mawaziri walikuwa wanajiandaa kupeleka bajeti bungeni.