Friday, November 18, 2011

Jaji Warioba; Ninyi Vijana nchi hii ni ya kwenu acheni kulaumu


Waziri Mkuu Mtaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
Mwanasiasa mkongwe na waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kuwa vijana hawapaswi kulaumu na badala yake wanapaswa kuchukua hatua za kuijenga Tanzania. Akitoa mada kwenye siku ya kumbukumbu ya Mwl Nyerere katika ukumbi wa NAH chuo kikuu Mzumbe mkoani Morogoro jumatano ya tarehe 16 mwezi huu, Jaji Warioba amenukuliwa akisema"vijana hampaswi kulaumu, nchi hii ni ya kwenu ni lazima mchukue hatua sasa za kuijenga Tanzania". Akizungumza kwenye mjadala huo ambao ulibeba kichwa cha habari "Mtazamo wa Mwl Nyerere kuhusu elimu ya juu". Katika mjadala huo pia wanazuoni mbalimbali walitoa mada ikiwa ni pamoja  na Dr Ishengoma(UDSM), Prof Mkude(Mzumbe), Emmanuel Kyando(Mwl Nyerere Butima Museum) na Dr Kapoka(Dodoma). Mjadala huo ambao ulikuwa wa kusisimua na washiriki hususani wanafunzi walipata muda wa kuchangia ambapo hawakusita kuweka wazi msimamo wao wa kutokubaliana na ubabaishaji mkubwa katika sekta ya elimu ya juu nchini
Baadhi ya wanafunzi  waliokuwa wakisambaza nyaraka na vipeperushi kwa washiriki wa mjadala huo
Dr Kapoka akitoa mada katika mjadala huo



No comments:

Post a Comment