Kile kitendawili cha baadhi ya workshops zinazofanyika Mzumbe University kukosa dhima kiasi cha wadau kuhoji kuwa zina faida gani? au zinamfaidisha nani? sasa kimeteguliwa baada ya Blog hii kujikusanyia ushahidi unaodhihirisha pasi na shaka wa baadhi ya workshops hizo kutumika kujenga mitandao ya kampeni. Blog hii imebaini jambo hili ikiwa ni takribani miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa MUSO ambao kadri muda unavyoenda na joto linazidi kupanda kwa kasi. Baadhi ya mbinu zinazotumika kujenga mitandao ya kampeni ni pamoja na wale wenye nia kupata wasaa wa kuzungumza hata kama hawana hoja za msingi lakini pia kumekuwa na tabia ya kukusanya namba za simu za wale wanaosadikiwa kuwa wapiga kura.
Tuesday, November 22, 2011
Breaking Newz; Waziri ataka wanafunzi waandamane kuwadai wenzao waliokopa walipe
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo
Peter Saramba, Arusha NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amewasihi wanafunzi wa elimu ya juu nchini kuandamana ili kushinikiza waliokopeshwa fedha za elimu miaka ya nyuma walipe ili wapewe wengine. Amesema wahitimu wengi walikopeshwa zaidi ya Sh21 bilioni ili kusoma kwenye vyuo mbalimbali, lakini baada ya kupata kazi wanakwepa kulipa mikopo hiyo. Mlugo alisema wanaosoma vyuoni sasa hawana budi kuandamana ili kuwashinikiza waliotangulia walipe fedha hizo ili ziweze kukopeshwa kwa wanafunzi wengine zaidi.
“Fedha hizo zilikopeshwa kwa wanafunzi wa elimu ya juu tangu utoaji wa mikopo ulipoanza mwaka wa masomo wa 2004/05 na kama zitapatikana zitaiwezesha Serikali kukopesha wahitaji wengi zaidi kuliko idadi ya sasa”, alisisitiza. Naibu Waziri Mulugo alisema hayo alipozungumza kwenye sherehe za mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Mount Meru eneo la Ngaramtoni, nje kidogo ya mji wa Arusha. Alisema baadhi ya wanaodaiwa fedha hizi wamefanikiwa kupata ajira rasmi huku wengine wakijiajiri wenyewe baada ya Serikali kugharamia elimu yao kupitia mikopo ambayo sasa hawataki kurejesha. “Tusiandamane (wanafunzi) kudai mikopo kutoka bodi ya mikopo pekee, sasa tuandamane pia kushinikiza waliokopeshwa sasa wanafanya kazi au kujiajiri warejeshe fedha walizokopeshwa ili ziingizwe kwenye mzunguko utakaowezesha wengi kufaidika,” alisema Mulugo akipigiwa makofi. Alisema Serikali ina nia ya dhati kuhakikisha wote wanaofaulu na kupata sifa za kujiunga na elimu ya juu wanapata fursa hiyo bila kujali uwezo kiuchumi wa mhusika, wazazi au walezi wake, lakini lengo hilo linakwamishwa na kipato kidogo na changamoto nyingi zinazohitaji kushughulikiwa na Serikali akitaja uboreshaji wa huduma za afya, miundombinu na huduma zingine za kijamii. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Naibu waziri huyo, idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaokopeshwa imekuwa ikiongezeka kila mwaka wa masomo ambapo mwaka 2004/5 , Sh 9.9 bilioni zilitumika kuwakopesha wanafunzi 16,345 kabla ya idadi hiyo kuongezeka hadi kufikia wanafunzi 42,729 mwaka uliofuata. Kuhusu maendeleo katika sekta ya elimu, hasa elimu ya juu, Naibu waziri huyo alisema nchi ilipopata uhuru mwaka 1961 kulikuwa na chuo kikuu kimoja pekee lakini sasa vipo vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki 41, kati ya hivyo 12 vikiwa vy umma na 29 vya binafsi huku udahili ukiongezeka kutoka wanafunzi 14 kwa wakati huo hadi 155,757 kwa sasa. Katika risala yao kwa mgeni rasmi, wahitimu 414 wa Chuo Kikuu cha Mount Meru waliishauri serikali kuwa pamoja na kuanzisha dawati la mikopo vyuoni, muda umefika wa kufikiria kuanzisha Ofisi za Kanda za Bodi ya Mikopo ili kurahisisha na kuongeza ufanisi kiutendaji.
Chanzo; Gazeti la Mwananchi
ST John Wafanya Mahafali
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Yohana (Saint John's University cha Dodoma katika mhafali ya
chuo hicho Novemba 5,2011. Kushoto kwake ni Mkuu wa Kanisa la Anglikan
nchini linalomiliki chuo hicho, Askofu, Dr. Valentino Mokiwa na kulia
kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Mstaafu, Dr. Donald Mtetemela.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Habari kwa hisani ya Blog ya wanavyuo Tanzania
Ms Asela Miho The pride of Mlimani
The
Chancellor of University of Dar es Salaam, Ambassador Fulgence Kazaura
(left) gives a reward to Ms Asela Miho (right) who graduated with a BA
degree and was the best overall student during the 4th graduation
ceremony of Dar es Salaam University College of Education (DUCE) on
Saturday. (Photo
by Yusuf Badi)
Monday, November 21, 2011
Mawazo gongana; Zamzam, Frank Mhilu &Lupakisyo Mwambinga
Zamzam anasema..."I appriciate t. Congrats to ministry of informtn, communication and technology. Rais umetendea haki wizara hii."
Lupakisyo Mwambinga anasema..."Huu utaratibu ulioanzishwa sikuhizi Green wa kutenganisha dirisha la watu wa msosi wa buku na dirisha la msosi ambao ni zaid ya buku kwa mtazamo wangu sijaupenda its like ubaguz fulani wa wateja na sisi ni wanafunzi."
Frank Mhilu anasema....ni dhahiri, maji mazito hayabebeki, hata pamba vilevile,...
najiuliza hizi kelele za ufisadi wa muso mwisho wake lini, au tulete dr toka india, nadhani ifikie mahali tuseme basi inatosha, viongozi lazima tuwajibike, wadau tunapaswa pia kuwajibika
safari hii hatuna masihara , tutawajibishana tu.
Sunday, November 20, 2011
Maoni ya Mhariri Leo; Acha Punch, acha Majungu, Lete Hoja Mezani
wabunge wa Mzumbe wakiwa Bungeni
Kwenu Wanamzumbe,Naandika tahariri hii nikiwa na majonzi makubwa kwa jinsi baadhi ya Wanamzumbe wanavyotaka kutuvuruga kwa kile kinachoweza kutafsiriwa kuwa ni "tamaa ya madaraka". Ikiwa takribani ni miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa MUSO tayari kampeni za chini kwa chini zimeanza (ingawaje ni kinyume na sheria) nimeshalisema hili siwezi kurudia tena walionisikia wameelewa na ambao hawataki kuelewa wangoje sheria itakapowakumbusha wajibu wao. Leo najitokeza tena kulaani vikali "zengwe" miongoni mwa wanamzumbe.
Hapa neno zengwe ni kuchafuana ambapo kunaweza kutafsiriwa kama kupigana punch na majungu, naam! mapuynch na majungu hayawezi kukubalika hata kidogo. Kama wasomi hatulikubali hili , hatulitaki na tutalilaani milele. Sisi ni wasomi hivyo tutaendelea kusimama katika ukweli ndiyo maana nasema kuwa umefika wakati sasa kwa Wanamzumbe kuanza kujitafakari na kuchukua uamuzi sahihi badala ya kuendelea kukumbatia "siasa za majitaka" Naam! iwe isiwe nitasema ukweli daima, leo nasisitiza kuwa Acha punch, acha majungu, lete hoja mezani!
Wabunge Wanavyoipa heko Mzumbe University
Na Mwandishi wetu Dodoma,
Blog hii imefanikiwa kutua mjini Dodoma na kufahamu mbivu na mbichi kuhusu waheshimiwa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania "kuifagilia" Mzumbe University kwa kile kinachodaiwa mafanikio ya kitaaluma , amani na utulivu wa chuo hiki huku wakichagiza "kwanini vyuo vingine visiige kutoka Mzumbe?"
Kutokana na hali hii, wataalamu wa maswala ya miradi na nertworking katika njanja za maendeleo na ujasiriamali chuoni hapa wanatoa wito kwa chuo kikuu Mzumbe kuitumia fursa hii kufanikisha agenda ya maendeleo huku wakisisitiza kuwa "Mzumbe must market its good reputation"
Katiba ya MUSO yaanza kusakwa kwa udi na uvumba
Onesmo Mpinzile mmoja wa wanasheria mahiri wa Mzumbe
Katika kile kinachoweza kudhaniwa kuwa ni mvutano wa kisheria tayari wadau wameanza kuisaka kwa udi na uvumba katiba ya MUSO ingawaje hawakuwa tayari kuieleza Blog hii nini hasa lengo lao? mfano siku ya jana pekee ni zaidi ya watu watano walifika MUSO office kuisaka katiba hiyo. Kumekuwa na tabia ya watu kuisaka katiba ya MUSO hasa inapofika wakati wa uchaguzi. Friday, November 18, 2011
The Untold Story about Professor Faustine Kamuzora
Do you know that Prof Kamuzora is also an Author? see the elite has number of titles in Economics, Social and Development. With experience of teaching for many years and many years of reading and doing research across the world prof Kamuzora is to be acknowledged as one of the distinguished Tanzanian writer in our times, yes!, Mzumbe University has a lot to be proud but having such elite and an author not only it is pride but also something the young generation ought to copy, read his titles click the link below http://www.kamuzora.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=47&Itemid=61
Mh Amon Chakushemeire; Kajiuzulu au ameandika barua ya kuomba kujiuzulu?
Mh Chakushemeire akizungumza kwenye baraza la mawaziri
Giza limetanda kufuatia taarifa za kujiuzulu kwa waziri wa Protocal wa MUSO Bw Amon Chakushemeire ambazo zimebaki kuwa "hazieleweki". Blog hii imefatilia kwa undani swala hilo na kubaini kuna uelewa mdogo wa mambo ya utawala miongoni mwa watu wanaoeneza taarifa hiyo kwa maana tunaomba tuweke wazi hapa kuwa alichofanya Mh Chakushemeire ni kuandika barua ya kuomba kujiuzulu kwa aliyemteua(rais) ambaye hata hivyo sheria zinamruhusu kuridhia ombi hilo au kukataa hivyo mpaka sasa bado rais wa MUSO hajatoa uamuzi wake kwa maana nyingine Mh Chakushemeire anapaswa kuendelea kuwajibika mpaka rais atakapotoa uamuzi wake vinginevyo kinachofanyika hapa ni kinyume cha sheria hivyo lazima lipingwe vikali nasi tunakuwa watu wa kwanza kutoa msimamo wetu juu ya hili kuwa HATUKUBALIANI NALO.
Prof Joseph Kuzilwa azungumza na Wanamzumbe kuhusu Changamoto zinazowakabili
Makamu mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe Prof Joseph Kuzilwa amezungumza na wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe( mwaka wa pili) kuhusu kero zinazowakabili siku ya jana. Taarifa ambazo Blog hii imezipata ni kuwa hatua hiyo ya Prof Kuzilwa imefuatiwa na ombi la wanachuo hao hasa mwaka wa pili walioomba kuonana na mkuu huyo wa chuo ambaye pamoja na mambo mengine walieleza kero mbalimbali kubwa likiwa ni swala la mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa pili, ambapo pamoja na swala hilo pia swala la Accomodation lilizungumzwa kwa undani ikizingatiwa kuwa sasa utaratibu wa TCU wa kudahili maelfu ya wanafunzi kwenye vyuo vingi hauna maana kwa mantiki kuwa wanafunzi wanaodahiliwa wanazidi hata uwezo wa baadhi ya vyuo kutoa huduma ya malazi kwa wanafunzi. Katika utatuzi wa swala hilo la mikopo Prof Kuzilwa ameridhia chuo kuwapatia wanafunzi hao shilingi laki tatu na nusu kila mmoja mpaka pale Bodi ya mikopo itakapowapatia fedha zao, pia amesisitiza kuwa swala la accomodation linamnyima usingizi professor huyo.
Jaji Warioba; Ninyi Vijana nchi hii ni ya kwenu acheni kulaumu
Waziri Mkuu Mtaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
Mwanasiasa mkongwe na waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kuwa vijana hawapaswi kulaumu na badala yake wanapaswa kuchukua hatua za kuijenga Tanzania. Akitoa mada kwenye siku ya kumbukumbu ya Mwl Nyerere katika ukumbi wa NAH chuo kikuu Mzumbe mkoani Morogoro jumatano ya tarehe 16 mwezi huu, Jaji Warioba amenukuliwa akisema"vijana hampaswi kulaumu, nchi hii ni ya kwenu ni lazima mchukue hatua sasa za kuijenga Tanzania". Akizungumza kwenye mjadala huo ambao ulibeba kichwa cha habari "Mtazamo wa Mwl Nyerere kuhusu elimu ya juu". Katika mjadala huo pia wanazuoni mbalimbali walitoa mada ikiwa ni pamoja na Dr Ishengoma(UDSM), Prof Mkude(Mzumbe), Emmanuel Kyando(Mwl Nyerere Butima Museum) na Dr Kapoka(Dodoma). Mjadala huo ambao ulikuwa wa kusisimua na washiriki hususani wanafunzi walipata muda wa kuchangia ambapo hawakusita kuweka wazi msimamo wao wa kutokubaliana na ubabaishaji mkubwa katika sekta ya elimu ya juu nchini
Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakisambaza nyaraka na vipeperushi kwa washiriki wa mjadala huo
Dr Kapoka akitoa mada katika mjadala huo
Jamii Forums Kulikoni? Nini Vyanzo vya taarifa zenu Kuhusu Mzumbe University?
Ikiwa takribani ni miezi mitatu tangu kwa mara ya kwanza Blog hii turipoti kile kinachoitwa "kuchafuliwa kwa Mzumbe University" katika mtandao wa habari wa Jamii Forums kwa kuiweka hewani ripoti ya uongo iliyolenga kumchafua Dr Mbwambo wa chuo kikuu Mzumbe, kwa mara nyingine mtandao huo umeibuka na uzushi mwingine wa kudai kuwa kuna mgomo umeiva Chuo Kikuu Mzumbe. Blog hii imefatilia kiundani na kufanikiwa kuunasa ujumbe huo ambao umepostiwa na mwandishi anayetumia jina bandia la "kipanga mlakuku" ujumbe huo unonyeshwa kuwa ulichapwa siku ya tarehe 25 october mwaka huu majira ya saa tano na dakika sita usiku, ujumbe huo unasomeka hivi
"Mgomo umeiva Mzumbe University: JK unahujumiwa?
Kwako Rais Jakaya Kikwete,Tunashindwa kuelewa vyanzo vya habari hii ambayo kwa akili za kawaida inaonyesha ni umbeya tu, lakini pia tuanshindwa kuelewa lengo la mtandao huo wa habari kuchapa habari ya "kipuuzi" kama hii? ambayo haina chanzo chochote, tunatumia jukwaa hili kutoa changamoto kwa mtandao huo wa habari kuacha mara moja kushabikia habari za kizushi na badala yake wajifunze kuwa watafiti badala ya kuendekeza udaku wa aina hii, au labda tuwahoji ni kosa kwa VC kufanya kikao na Wanafunzi? hakika hili uzushi wa kipuuzi wa aina hii haukubaliki!
Ni hivi punde mdogo wangu ambaye amechaguliwa kujiunga na chuo kikuu Mzumbe amenipigia simu na kunieleza jinsi management ya chuo kikuu Mzumbe wakiongozwa na Prof Kuzilwa na Prof Kamuzora jinsi wanavyosuka mgomo kwa lazima. Tuhuma hizi zinachochewa na kitendo cha chuo hiko kwa kushirikiana na TCU kujaza maelfu ya wanafunzi kushinda uwezo wa chuo kiasi kwamba sasa "kuna vuta nikuvute kwenye maswala ya accomodation"
Mpaka sasa inaelezwa kuwa historia ya kutogoma ya chuo kikuu Mzumbe ambayo JK amekuwa akijivunia huenda ikafutika muda wowote kutoka hivi sasa kutokana na tishio la mgomo huo ambao yaelezwa muda wowote waweza kuanza.
Hapa ndipo nataka kumuuliza JK kuwa yeye kama rais haoni kuwa anahujumiwa na maprofessor hawa? je Jk yupo tayari Mzumbe kugeuka "Mlimani?" SOMA HABARI KAMILI BOFYA HAPA;http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/185951-mgomo-umeiva-mzumbe-university-jk-unahujumiwa.html
Prof Kamuzora; Si Kweli Kwamba tunalea watu wasio na maadili
Prof Faustine Kamuzora akiwa jijini New York nchini Marekani katika jengo la World Trade Centre
Siku ya tarehe 16 mwezi huu ambayo ilikuwa ni siku maalumu ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere katika chuo kikuu Mzumbe , sambamba na sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Blog hii ilimtafuta professor Kamuzora na kufanya naye mohojiano katika hotel ya Lumumba, soma zaidi...........
MUSO Link; Hongera prof Kamuzora na wanamzumbe wote kwa kuadhimisha siku hii, je wewe unaizungumzia vipi siku hii?
Prof Kamuzora; Asante , kwanza napenda nikumbushe kuwa kwa chuo kikuu Mzumbe siku hii ya Mwl Nyerere huadhimishwa kila mwaka sio mwaka huu tu, lakini pia naweza kusema kuwa imekuwa ni siku nzuri watu wamepata muda wa kujadili kuibua mawazo na kuchangia maswala mbalimbali ikizingatiwa kuwa Mada ya leo ilihusu mtazamo wa Mwl Nyerere katika elimu ya juu.
MUSO Link; Kumekuwa na mtazamo kuwa siku hizi wasomi wamekuwa hawana maadili tofauti na enzi za Mwl Nyerere, je wewe unalizungumziaje hili?
Prof Kamuzora; Ndugu mwandishi si kweli kwamba tunafundisha au kulea watu wasio na maadili, ukweli ni kuwa hat leo hii kuna watu ambao ni waaminifu "clean" tena wana maadili halikadhalika kuna watu ambao hawana maadili, hivyo si kweli kabisa kuwa watu wote wa kizazi hiki ni waovu.
MUSO Link; Ungependa kuwaambia nini wanamzumbe na watu wengine kuhusiana na siku hii ya Nyerere?
Prof Kamuzora; Kwanza wanamzumbe wanapaswa kufahamu kuwa hii ni siku muhimu sana ya kujadili maswala mbalimbali pia watanzania kwa ujumla wanapaswa kujadili mitazamo ya baba wa Taifa, kuipima lakini pia watu wanapaswa kuzingatia zama tulizopo "era" kwa maana zama pia zimebadilika na hata mambo yanabadilika pia.
MUSO Link; Asante Professor na nakutakia kazi njema
Prof Kamuzora; Asante pia.
Thursday, November 17, 2011
Fred Kanuti Valentino; Mwanamzumbe , Ndugu Yetu lala Mahali Pema Peponi!
Marehemu Fred Kanuti
Tarehe 26 mwezi wa 10 mwaka huu Jumuiya ya Wanamzumbe ilipatwa na majonzi mazito kama sio mtikisiko mkubwa kufuatia kuaga Dunia kwa mwanafunzi mwenzetu wa mwaka wa tatu ndugu yetu Fred Kanuti Valentino kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya damu, Blog hii ilikuwepo kwenye mazishi ya ndugu yetu huyu yaliyofanyika Kimara Temboni jijini Dar es salaam, fatilia picha zifuatazo ili uelewe kilichojiri....;
Mwili wa ndugu yetu Fred ukiwa kwenye jeneza tayari kwa kupewa heshima za mwisho
Watu wakitoa heshima za mwisho
Mama huyu akimlilia ndugu yetu Fred ilikuwa ni huzuni kubwa
Huyu ni Vice President wa MUSO Happiness Joseph akimlilia Fred
Baba Dean akiwa na huzuni kubwa
Hapa ilikuwa kanisani , Ibada ya mazishi ikiendelea
Jeneza likishushwa kaburini
Jeneza likiwa ndani ya kaburi
Msalaba ukiwekwa juu ya kaburi
Kaburi la ndugu yetu Fred likiwa limepambwa kwa maua na mishumaa kuashiria watu walivyompenda
Hapa ndipo alipolala mpendwa wetu Fred Kanuti Valentino.
KWA NIABA YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU MZUMBE BLOG HII INATOA POLE KWA NDUGU WA MAREHEMU, DAIMA TUTAMKUMBUKA FRED, AMEN!
Sunday, November 13, 2011
Hoja yetu; Tatizo si Kampeni bali Muda Haujafika
Na Mhariri Mkuu,
Nianze na nukuu ya waziri mkuu wa MUSO Bw Benson Futte aliyowahi kuitoa wakati akizungumza bungeni aliwahi kunukuliwa akisema "uongozi na dhamana na hakika ni kazi kubwa inayohitaji kujitoa kuwatumikia watu" swadakta haya hakika ni maneno ya busara na hayakusemwa kimakosa ila kinachotusikitisha ni jinsi baadhi ya watu walivyoanza kampeni kabla ya muda. Ukirejea mtiririko wa mantiki tunayojenga hapa utabaini kuwa hatuwapingi wanaotaka uongozi , abadani hatupingi kampeni ila tunachosema ni kuwa TATIZO SI KAMPENI BALI MUDA HAUJAFIKA.
Tunayasema haya siyo kwa majungu bali tukiwa na uhakika wa zaidi ya asilimia mia moja kutokana na utafiti wa muda mrefu ambao umebaini kuwa kuna baadhi ya watu wenye lengo la kugombea urais wameanza kampeni kabla ya wakati hivyo tunachukua nafasi hii kuwakanya na kuwataka waache mara moja harakati hizo ambazo ni kinyume cha sheria badala yake tunawataka wangoje muda mwafaka.
Nianze na nukuu ya waziri mkuu wa MUSO Bw Benson Futte aliyowahi kuitoa wakati akizungumza bungeni aliwahi kunukuliwa akisema "uongozi na dhamana na hakika ni kazi kubwa inayohitaji kujitoa kuwatumikia watu" swadakta haya hakika ni maneno ya busara na hayakusemwa kimakosa ila kinachotusikitisha ni jinsi baadhi ya watu walivyoanza kampeni kabla ya muda. Ukirejea mtiririko wa mantiki tunayojenga hapa utabaini kuwa hatuwapingi wanaotaka uongozi , abadani hatupingi kampeni ila tunachosema ni kuwa TATIZO SI KAMPENI BALI MUDA HAUJAFIKA.
Tunayasema haya siyo kwa majungu bali tukiwa na uhakika wa zaidi ya asilimia mia moja kutokana na utafiti wa muda mrefu ambao umebaini kuwa kuna baadhi ya watu wenye lengo la kugombea urais wameanza kampeni kabla ya wakati hivyo tunachukua nafasi hii kuwakanya na kuwataka waache mara moja harakati hizo ambazo ni kinyume cha sheria badala yake tunawataka wangoje muda mwafaka.
Subscribe to:
Posts (Atom)