Tuesday, October 4, 2011

Barua Ya Wazi Kwa Mh Uswege na Futte; First Year Wajengwe Kisaikolojia!


Tunaandika Barua hii maalumu kwenda kwa rais wa MUSO pamoja na Waziri mkuu kutoa wito kwa viongozi hao wa MUSO kuwajenga kisaikolojia wanafunzi wa first year wanaotegemewa kuwasili chuoni hapa week chache zijazo.

Tunayasema haya kutokana na "mchecheto" uliowaangia baadhi ya mwaka wa kwanza ambao tumefanikiwa kuongea nao, hatupingi furaha yao kupangiwa Mzumbe la hasha! bali tunachojaribu kupinga hapa ni ile furaha kupitiliza kiasi cha kushindwa kuuona ukweli. hii ni moja lakini cha pili ni baadhi ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza kumezeshwa mambo ya "kipuuzi" kuwa eti Mzumbe ni chuo kigumu sana.

Magwiji wa falssafa waliwahi kusema kuwa "You Are What You Think" kwa mantiki hiyo mawazo haya hasi ya kufeli yaweza kuwafanya baadhi yao wakafeli kweli ndiyo maana tunaandika kutoa wito kwa viongozi hao wakuu wa MUSO kufanya juhudi za dhati kuhakikisha ndugu zetu hao wa mwaka wa kwanza wanajengwa kisaikolojia ili waweze kusoma na kuishi vizuri hapa chuoni Mzumbe.

No comments:

Post a Comment